Ilikua inajulikana kwamba mchezaji Sanchez ana tatizo la calf peke yake, Wenger ametoa taarifa zaidi kwamba mchezaji huyo ana matatizo zaidi ya hilo. Boss wa Chile Antonio Pizzi amesema kwamba Sanchez atabaki kwenye kikosi chao na ana matumaini kwamba atakua fit kwenye mechi dhidi ya Uruguay.
Kuhusu hii ishu Wenger alisema kwamba,“Nimepata text jana usiku kuhusu majeraha zaidi ya Sanchez. Timu ya Chile imesafiri bila yeye ili kumuacha apumzike kwa ajili ya mechi dhidi ya Uruguay. Tunahitaji watu wetu wa timu ya matibabu wapate access kumfanyia uchunguzi Sanchez kabla Chile haijafanya jaribio litakaloleta madhara zaidi ambayo yanaweza kumsumbua kwa miezi mingi ijayo”.
Wenger aliongeaza.“Hii ni muhimu sana kwa timu ya taifa na club yake, siku zote Sanchez anataka kucheza lakini afya yake ni muhimu kwa pande zote mbili na lazima izingatiwe”