1. Muhammadu Buhari wa Nigeria
Alisoma Shule ya msingi Daura na Mai’adua huko Katsina State, Nigeria Kaskazini. Na kisha kujiunga na shule ya Katsina Model mwaka 1953, na badae sekondani ya kitongoji cha Katsina ambayo kwa sasa ni chuo cha serikali mwaka 1956 – 1961.
2. Dennis Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Congo
Alipokea mafunzo yake katika chuo cha Ualimu, Dolisie Nairi. ameendesha nchi kuanzia enzi za Brazzaville mwezi oktoba 1997.
3. Isaias Afwerki wa Eritrea
Licha ya kwamba hakumaliza masomo yake ya Sekondari, Rais wa Eritrea Isaias Afwerki anaongoza vizuri tu nchi yake. Japo katika rekodi nyingi inaonekana alitunukiwa cheti kutoka shule ya Prince Makonnen lakini hakuweza kusoma masomo ya Chuo kwasababu hakupata alama za kutosha na baadae akajiunga na kuwa mwanaharakati wa kuikomboa Eritrea
4. Paul Kagame wa Rwanda.
Rais Kagame alianza shule ya msingi karibu kabisa na kambi ya wakimbizi alipofunzwa Kiingereza na utamaduni wa Kiganda. Na alipofiwa na Baba yake miaka ya 70, maendeleo yake shuleni yakadhoofika. Na katika harakati za yeye kupenda siasa aliishia kuahirishiwa masomo yake na kumaliza tofauti na wenzie katika shule ya sekondari ya zamani ya Kampla.
5. Yahya Jammeh kutoka Gambia.
Ni maarufu sana kwa mafunzo aliyopata Jeshini. Alipomaliza tu elimu yake ya Sekondari the Gambia High School in Banjul alijiunga na Jeshi la Taifa la Gambia mwaka 1984 na kupandishwa cheo cha Luteni mnamo mwaka 1989 na baadae kuwa Mkuu wa polisi kabla ya kuwa Rais wa Gambia.