MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Taratibu Phidaya akasimama, akanisogelea huku machozi yakimwagika. Nikataka kumkumbatia, ila akanizuia, nisifanye hivyo.
Kofi
zito kutoka kwa Phidaya likatua shavuni mwangu, lililo mfanya Shamsa
kustuka. Phidaya akaachia msunyo mkali na kumshika mkono Jack.
"Junio tuondoke"
Phidaya alizumgumza kwa hasira, na kuanza kuondoka na mwanaye, wakijichanganya katikati ya watu walio kusanyika hapa.
ENDELEA
Sikuhofia kukatiza katikati ya watu, kuwafwata Phidaya na mwanagu
Junio. Furaha moyoni nwangu ikawa imezaliwa upya kuiona familia yangu.
Iliyo nigharimu maisha yangu katika kuitafuta hadi leo kuitia machoni
kwa mara ya pili, ukiachilia siku ya kwanza Junio alivyo zaliwa mbele ya
macho ya watu wengi akiwemo Shatani John na Victoria.
"Phidaya, Phidaya"
Nilimuita
Phidaya niliye mkaribia, kumfiki. Akasimama na kunitazama kwa macho
makali sana, yaliyo jaa hasira huku machozi yakimwagika taratibu.
"Unakwenda
wapi mke wangu, kumbuka nimehangaika kwa ajili yako, nimejitolea maisha
yangu kwa ajili yako na mwanangu. Kwa nini unanikasiriki, kosa langu ni
nini haswa?"
Nilizungu huku machozi yakianza kunitiririka.
"Nimekua muuaji kwa ajili yako, nimefanya kila niwezalo kufanya kwa ajili yako, ila umaona yote hayana dhamani si ndio?"
"Eddy
nyamaza. Nilikuomba usioe, ila kwa nini ulioa. Umeniacha nahangaika,
naishi maisha ya kitumwa na mwanangu. Tumekua watu wa kubadilisha majina
kwa ajili yako. T...."
"Phidaya
mimi sijaoa mwanamke yoyote, nilijitoa kufa na kupona kuwakomboa nyinyi
mukiwa kwenye maroli kwenda kuuzwa nchi za nje. Nimefanya kosa?"
"Eddy acha uongo, haukuwa wewe, uliye tuokoa, Umemuoa mwanamke aliye nidhalilisha na kuniita mimi malaya, mimi?"
"Phidaya,
achana na hayo maneno. Njoo tukamlee Junio. Twende tukaishi kwa amani
na upendo. Unatambua ni mazingira gani ulimzaa Junio, huku na mimi
nikiwa kwenye tabu gani."
"Junio sio mwanao, ni mwanangu peke yangu. Junio twende zetu"
Phidaya alizungumza huku akimshika mkono Junio, na kumvuta waondoke ila Junio akagoma kwenda popote.
"Mama
uliniambia mtu, akiniuliza baba yangu ni nani, nimuambie simjui. Ila
Eddy ni baba yangu, mara ngapi ulikua ukimpigis simu. Anamapenzi ya
dhati na sisi. Mama nimechoka kuishi maisha haya ya ukimbizi. Mpe baba
nafadi yake, aonyeshe ni jinsi gani anavyo tupenda."
Japo
Junio kiumri ni mdogo, ila maneno aliyo yazungumza huku akilia
yakanifanya mwili wangu kusisimka. Phidaya akamtizama Junio kwa macho ya
mshangao, kisha akanitazama na mimi.
Nikafungua vifungo vya shati langu, nikakivua na kumpa Shamsa anishikie.
"Majeraha
yote haya, nikwaajili ya kuiokoa familia yangu. Mwili wangu haukua na
dhamani juu ya kuziokoa nafsi zenu. Msikilize anacho sema mwanao.
Anahitaji malezi yetu sote. Tafadhali mke wangu, rudi mikononi mwangu au
unataka mwanangu aendelee kuishi maisha haya ya shida. Tazama jinsi
sura yake ilivyo umuka kwa kupigemwa na wezake. Je unataka awe hivi kila
siku?"
Nilizungumza
kwa uchungu, huku nikipiga magoti chini, sikujali ni idadi ngapi ya
wagu walio tuzunguka wakitushangaa. Junio akamshika mkono mama yake.
"Mama, unanifundisha niwe mpatanishaji kwa walio gombana. Mshike baba mkono anakupenda"
Phidaya aliendelea kulia kwa uchungu, sura yake yote ikabadilika na kuwa na uwekundu fulani, kutokana na kulia kwa uchungu sana.
"Nakuomba mama, patana na baba anakuhitaji bado"
Maneno
ya Junio yakamlainisha Phidaya. Taratibu Phidaya akarudi sehemu niliyo
piga magoti, na yeye akapiga magoti chini, huku akilia. Kwa nguvu
akanikumbatia. Nikamvuta Junio wangu, naye nikamkumbatia huku sote
machozi ya furaha yakitumwagika. Watu walio tuzunguka wakaanza kupiga
makofi, yafuraha. Shamsa akabaki akinikonyeza huku akitabasamu.
"Nakupenda mume wangu"
"Nawapenda wote"
Tukaendelea kukumbatiana kwa furaha.
"Eddy muda"
Shamsa
alininong'oneza baada ya kuona tunakumbatiana sana. Tukanyanyuka,
nikambeba Junio wangu ambaye kwa sasa anatarajia kufikisha umri wa miaka
mitano.
"Nitakufanyia sherehe kubwa siku ya kuzaliwa kwako"
Nilimuambua
Junio, huku tukielekea kwenye ofisi kukamilisha taratibu zote za
kuwachukua Phidaya na mwanangu, na kuwa mikononi mwangu.
"Kweli baba"
"Ndio unataka ifanyikie wapi?"
"Mama kule kwa kina yule mchezaji uliye ninunulia mpira wenye jina lake ni wapi?"
"Brazil"
"Ndio, dady nataka huko huko na mimi nikawe mchezaji mpira"
"Usijali mwanangu, unaweza kucheza mpira?"
"Ndio baba nataka niwe kama Ronaldo"
"Sawa mwanangu utakuwa, tena kabla sijasahau, huyu ni Shamsa, mdogo wangu. Kwa sasa atakuwa dada yake Junio"
"Kweli dady?"
"Yeah"
Nikambusu Junio kwenye paji la uso, jambo lililo zidisha furaha kati yetu sote wanne.
***
Kitendo cha ndege kutua kwenye uwanja wa ndege nchini Brazil, likawa ni
jambo la kumshukuru Mungu, sote tukafungua mikanda ya siti zetu tulizo
kalia, ikiashiria kwamba safari yetu immefika mwisho. Tukatoa mabegi
yetu ya nguo, katika sehemu tulipo yaweka. Tukatoka ndani ya ndege kama
abiria wengine. Tukafika eneo la kukaguliwa, tukafanikiwa kupita pasipo
kusumbuliwa, juu ya hati zetu za kusafiria. Tulizo zikata nchini Kenya
tukisaidiwa na rafiki wa Smith, aliye tukutanisha naye kipindi tunatoka
Tanzania mimi na Manka, ambaye hadi sasa sijui yupo wapi.
Kwa msaada wa ramani tuliyo pewa na rafiki wa Smith, juu ya miji yote
mikuu nchini Brazili, ikatusaidia kutufikisha kwenye hoteli tuliyo
kusudua kufikia tangu tukiwa nchini Kenya. Hoteli hii inapatikana
pembezoni mwa fukwe za bahari zijulikanazo kwa jina la 'Copar Carban'.x
Sehemu
tuliyo chukua kwa ajili ya makazi ya wiki mbili, ina vyumba vitatu,
seble, kubwa pamoja na xjiko kubwa. Kila chumba kimejimudu kwa huduma
zote muhimu kama choo na bafu.
"Eddy hapa umelipia bei gani?"
Phidaya alizungumza huku akikagua kagua chumba chetu cha kulala, chenye hadhi ya nyota tano.
"Kwa siku ni dola elfu sabini"
"Mmmmm kwa chumba hiki au?"
"Kwa sehemu yote, hii"
"Kweli una pesa ya kuchezea, hii ni birthday ya mwanao mambo ni haya, Je siku ya ndoa yetu itakuaje"
"Ndio ujiulize sasa, nataka kuihakikishia dunia nzima kwamba ninakupenda mke wangu"
Phidaya
akanikimbilia, nilipo simama. Akanirukia na kuning'inia kifuani kwangu.
Huku miguu yake akiipitisha kiunoni mwangu na kuikutanisha nyuma.
"Wewe ni mwanaume jasiri, i wish wanaume wote wangekua kama wewe. Ninaamini furaha ingepatikana katika ndoa nyingi."
"Ni wachache wenye moyo kama wangu. Ila kikubwa nimekupata wewe na mwanangu, ninaamini furaha itarudi upya"
Phidaya
hakusita kuusogeza mdomo wake, karibu na mdomo wangu. Akanitazama kwa
muda, kisha kwa haraka akaanza kuunyonya mdomo wangu. Kutokana na nguvu
nilizo nazo, sikuweza kutetereka, kwani fujo anazo zifanya Phidaya
mdomoni mwangu, huku nikiwa nimembeba, mtu unaweza kuanguka chini.
Nikamlaza kitandani, huku akiendelea kuninyonya lipsi zangu, mikono
yangu nikaishusha kifuani mwake, na kuanza kuzichezea chuchu zake. Kwa
raha anazo zipata Phidaya, akajikuta akifumba macho yake. Nikazidi
kuutadhimini uzuri wa Phidaya. Hapa ndipo nilipo jilaumu, kwa nini
nilikua na magubegube, Sheila na Madam Mery. Kwa kupitia kioo kikubwa,
kilichopo kwenye kitanda chetu. Nikamuona Junio akiwa amesimama mlangoni
huku akiwa ameshika mpira alio nunuliwa na mama yake. Mdomo wake akiwa
ameulegeza akishangaa tunacho kifanya.
Nikamuona
naye Shamsa, akisimama nyuma ya Junio, wote walikua na safari ya
kuingia chumbani kwetu. Shamsa akamfumba macho Junio, aliyeganda
akishangaa kama mshumaa wa pasaka. Shamsa akamyanyua Junio taratibu huku
akiwa amemfumba macho. Akanikonyeza, na mimi nikamuonyesha ishara ya
dole gumba kwa kutumia mkono wa kulia huku mkono wa kushoto akiendelea
kuchezea chuchu za Phidaya. Shamsa akatabasamu, taratibu akaurudishia
mlango wetu, huku mkono alio mziba macho Junio akiutumia kuufungia
mlango, na kumpa fursa Junio kushangaa vya mwisho mwisho.
"Eddy ni nini hicho?"
Phidaya aliniuliza huku akiyafumbua macho, yake kutazama kila kona ya chumba.
"Kitu gani?"
"Kilicho gusa mlango"
"Hakuna kitu bby"
Phidaya
akapotezea, na kuendelea na zoezi la kuunyonya mdomo wangu. Huku kila
ma}ra akihakikisha ananigusa kila kona ya mwili wangu. Tukavuana nguo
tulizo zuvaa, na kubaki kama tulivyo zaliwa.
***
Sote tukajikuta tukiwa tumechoka, kutokana na mechi tuliyo ipiga, saa
ya ukutani inatuonyesha ni saa tisa alasiri. Huku mechi tukiwa tumeianza
saa sita mchana, uzuri ni kwamba tulifika nchini Brazil, saa kumi na
moja alfajiri na hadi tunafika hotelini, ilikua saa sita kasoro.
Phidaya akashuka kitandani huku, akiyumba yumba
"Eheee leo Eddy umenikomoa, hadi miguu imepoteza nertwork. Kweli wewe ni baba Junio. Sikukosea kuzaa na wewe"
"Hata wewe ulinikamia, hapa nina kiu"
"Kiu ya nini tena? Kama ni yakitandani ahaaa usije ukaniua bure"
"Kiu ya maji"
"Ahaa ndio umalizie matamshi yako"
Phidaya
akafungua friji, akatoa chupa ya maji, akanirushia kisha yeye akaingia
bafuni. Sikuamini kwamba ipo siku nitakuja kumpata mke wangu. Hapa ndipo
nilipo tambua, ukijibidiisha kwa kila jambo zuri, mwisho wake nifuraha.
"Eddy Eddy"
Phidaya
aliniita kwa sauti ya juu, iliyo nistua. Nikanyanyuka haraka na
kukimbilia bafuni. Nikamkuta akiwa amesimama kwenye bomba linalo mwaga
maji kwa mfumo wa kama mvua.
"Una nini mke wangu"
"Hahahaaaa, kumbe unanipenda. Nimekuita tuje kuoga."
Phidaya akanivuta karibu yake, na kunikumbatia.
"Kelele nyingine tutakuja kuuana kwa....."
Phidaya akauwahi mdomo wangu kwa kukiwekea kidole chake, ili nisimalize kuzungumza nililo hitaji kuzungumza"
"Shiiii kila mtu na chake. Nisipo kutania wewe nimtanie nani?"
"Ahaa..."
Fhidaya akaniziba mdomo wangu kwa mdomo wake. Busu alilo nipa likanifanya nikae kimya.
"Hii ni siku yetu, sitaki kelele zako"
"Sawa bosi Phidaya"
"Am not your boss"
"But."
"Am your wife, mother of your child"
"Mama Junio"
"Ndio maana yake"
Tukamaliza kuoga, kisha tukarudi chumbani, Phidaya akanichagulia nguo
za kuvaa, zinazo endana na mazingira ya kupungia upepo kwenye fukwe.
Tukatoka sebleni. Hatukuwakuta Shamsa na Junio, tukatazama kwenye vyumba
vyao ila hatukuwaona.
"Watakuwa kwenye fukwe"
"Sasa watakwendaje pasipo kutuaga"
Phidaya
alizungumza huku akiwa amekasirika, akafungua mlango na kutoka,
nikabaki nikicheka, kutokana hakulishuhudia tukio la Junio na dada yake.
Tukafika kwenye fukwe iliyo jaa watu wengi. Tukawakuta wakicheza mpira
na watoto wengine, huku, Shamsa akiwa refa wao.
Junio alivyo tuona akakatisha mchezo na kuja tulipo huku akifwatana na Shamsa.
"Mbona mumeondoka bila kutuaga?"
"Mama tuliwaku..."
Shamsa akawahi kumziba mdomo Junio huku akitabasamu. Mimi nikawa nimeielewa maana ya Shamsa kumziba mdomo Junio.
"Wangetuaga saa ngapi mke wangu wakati mlango tulifunga?"
Phidaya akashusha pumzi, akibaki anatushangaa sote.
"Mumeshinda ninyi leo"
Sote tukabaki tukimcheka Phidaya aliye nuna, kisa tu hajaagwa na wanae.
Usiku ukapita salama salmini, kulipo pambazuka tukaanza mizunguko ya
kununua vitu kwa ajili ya siku ya kuzaliwa ya Junio, iliyo bakisha siku
mbili hadi ifike. Tukazunguka maduka kadhaa, hadi inafika mchana
ikatulazimu kuingia kwenye mgahawa mmoja kupata chakula cha mchana.
"Jamani mumesha wahi kula hivyo vyakula mivyo agiza au ndio ushamba. Musije matumbo yakawauma, bado tuna mizunguko mingi"
Nilizungumza
kwa kuwatani. Kila mmoja akajibu anauhakika na chakula alicho kiagizia
hakita mletea madhara yoyote. Kila mtu akaletewa chakula chake, Phidaya
akawa ndio mtaja majina ya vyakula vilivyo wekwa mezani kutokana na
kuvifahamu vizuri.
Tukamaliza kula, nikalipa pesa wanayo tudai. Tukatoka na kuvuka barabara upande wa pili, kwenda kwenye duka moja la viatu.
"Dady nimeusahau mpira wangu"
"Wapi?"
"Pale chini ya meza, tuliyo kaa"
"Chagueni viatu, ngoja nikachukue huo mpira.
Nikawaacha
mimi nikarudi kwenye mgahawa tulio toka. Nikafika kwenye meza, tuliyo
toka kukaa muda si mrefu. Nikaukuta mpira wa Junio anao upenda kuliko
kitu chochote. Kitendo cha kunyanyuka, nikamshuhudi Sheila na John
wakiingia ndani ya mgahawa huu, wakitafuta sehemu ya kukaa, pasipo wao
kuniona.
Nikabaki nikiwa ninawashangaa, hadi wakapata sehemu ya kukaa pasipo wao
kuniona. Nafsi moja ikawa inanishawishi kwenda walipo kaa, ila nafsi
moja ikawa inanikatiza kufanya ujinga kama huo kwani sehemu nilipo iacha
familia yangu si salama kabisa. Na linaweza kuwa kosa kubwa sana la
kupotelewa tena na familia yangu. Nikaendelea kuwatazama jinsi wanavyo
onekana ni wenye furaha sana. Sheila hakuonyesha dalili yoyote kuwa na
ujauzito kutokana na nguo alizo zivaa zimembana sana mwili wake.
Nikapiga
hatua hadi mlangoni, nikasimama huku nikifikiria ni nini nimfanyie John
kwa yale yote aliyo nitendea kipindi nikiwa mikononi mwake. Jasho
lililo changanyika na hisia kali ya asira taratibu likaanza kunimwagika.
Huku likiambatana na mapigo ya moyo yalio nifanya nijihisi vibaya. Kwa
haraka hali hii ninakumbuka ilinitokea kipindi nikiwa ofisini mwa balozi
wa Marekani nchini Afrika Kusini, pale alipo ingia John na Victoria,
wakiwa miongoni mwa wageni walio alikwa na balozi huyo.
Nikajikaza
na kutoka nje ya mgahawa. Nikatafuta sehemu nikashika nguzo moja kati
ya nguzo kadhaa zilizopo pembezoni mwa barabara. Kizunguzungu kilicho
nishika gafla taratibu kikaanza kupungua taratibu, huku jasho
likiendelea kunimwagika usoni. Kitu kilicho nichanganya ni matone kazaa
ya damu, yaliyo anza kutoka puani.
"Ohhh Mungu wangu, nini hichi?"
Nilijisemea huku nikiyatazama matone ya damu yanayo dondoka chini.
"Sir you need help?"(Muheshimiwa unahitaji msaada)
Askari
mmoja anayelinda kwenye mgahawa huu, aliniuliza baada ya kunitazama
tangu nikiwa ninatoka nje, mpaka ninashikilia nguzo hii ya taa za
barabarani.
"I need water"(Nahitaji maji)
Akaingia
ndani ya mgahawa, akatoka akiwa ameshika chupa ya maji. Akaifungua, na
kunikabidhi. Nikajimwagia kichwani kidogo, kisha nikanawa usoni kutoa
damu zilizo churuzika kutoka puani mwangu.
Nikasubiri
kama dakika tano, mwili kidogo ukapata nguvu za kutembe. Nikamshukuru
mlinzi, nikavuka barabara na kwenda kwenye duka nilipo waagiza Phidaya
awachagulie wanae viatu. Nikawakuta wakiendelea kuchagua chagua viatu
wanavyo vipenda.
"Mbona umelowa kichwani?"
Phidaya aliniuliza huku akinigusa gusa kichwani mwangu.
"Kichwa kidogo kilikua kinaniuma, ndio nikanawa kichwani"
Ilinibidi
kumdanganya Phidaya kwa maana vita yangu na John, nitaka niimalize mimi
nwenyewe japo Phidaya naye alihusika katika mateso yote tuliyo
sababishiwa na John.
"Hiii damu nayo imetoka wapi?"
Aliniuliza huku akinishika kwenye kifua changu akinionyesha matone kadhaa ya damu.
"Dady hapo je, nimependeza?"
Junio
alisimama mbele yetu, huku akiwa amevalia viatu aina ya Supra, huku
akiwa ameshika miwani iliyo endana na viatu alivyo vivaa, ikanilazimu
kumjibu Junio kwanza na kulikwepa swali la Phidaya.
"Yeah umetokelezea mwanangu."
"Je nikivaa hii miwani?"
"Umekua kama Michael Jackson"
Junio akanifwata nilipo simama, tukagonganisha mikono, akaondoka akiwa amefurahi sana.
"Huo ubishoo mwanao ameridhi kwa nani?"
"Nikuulize wewe baba mtu, mtoto anapenda kuvaa vitu vizuri kama anajua kuvinunua"
"Muache bwana ndio muda wake huu wa kupendeza"
"Sawa tuachane na hayo, nijibu hizo damu umetoa wapi?"
"Tutazungumza nyumbani"
"Eddy umetoka kupigana?"
"Hapana mke wangu"
"Ila ni nini?"
"Sijapigana mke wangu. Hembu nenda ukawaambie hao wanao wafanye haraka turudi hotelini. Sijisikii vizuri"
Phidaya akanitazama machoni kwa umakini, kisha akawafwata Shamsa na Junio, sehemu walipo.
Nikasimama
kwenye ukuta wa vioo wa hili duka ulio elekea sehemu ulipo mgahawa,
nilipo waacha John na Sheila. Dakika kama tatu, nikamuona John na Sheila
wakitoka kwenye duka hilo. Wakaingia kwenye gari moja yakifahari iliyo
simama baada ya wao kusimama nje.
Nikastukia
nikiguswa kwa nyuma, nikageuka na kumkuta Phidaya akiwa amesimama nyuma
yangu, huku macho yake yakielekea lilipo gari walilo panda Jonh na
Sheila.
"Unashangaa nini?"
Phidaya aliniuliza.
"Nashangaa magari"
"Alafu ile gari nimeipenda"
"Iipi?"
"Ile lililo ondoka nje ya mgahawa"
Nikagundua Phidaya hajamuona John, laiti angemuona asinge zungumza maneno kama haya.
"Nitakununulia"
"Mmmm ila inaonyesha ni gari la gharama sana"
"Hakuna shida, tutatafuta tununue na sisi, lakwetu"
"Haya njoo uwalipie hawa wanao viatu vyao walivyo vichagua"
Nikafika
sehemu ya kulipia nikakuta viatu vya Junio na Shamsa vikiwa vimepangwa
kwenye meza moja kubwa na kila mmoja amechagua pea ya viatu zaidi ya
kumi.
"Eheee vyote hivi munakwenda kuvaa au kuweka mapambo?"
"Kuvaa"
Shamsa alinijibu huku akitabasamu.
"Mmm haya bwana"
"Ila kaka ndio watoto hao, usilalamike"
Jamaa muhudumu alizungumza kiswahili nakutufanya sote tushangae.
"Unajua kiswahili?"
"Ndio kaka, nilikulia Nairobi Kenya. Ila kaka familia yako ipo vizuri sana"
"Asante"
"Huyo mwanao wa kike amefanana sana na mama yake na huyo wa kiume ni chata yako kabisa."
"Etieer ehee"
"Ndio, hongera sana, umejua kuchagua."
Jamaa,
alikua mzungumzaji sana, ila kusema ukweli Shansa anafanana sana na
Phidaya, kuanzia rangi za mwili hadi sura zao. Japo mara kadhaa, Phidaya
alikua akikataa hajafanana na Shamsa.
"Ni kiasi gani nadaiwa?"
Janaa akaminya batani ya mashine iliyo mbele yetu. Ikatoa bei ya pamoja ya viatu vyote.
"Hembu weka hiyo miwani kwenye meza"
Junio akaweka miwani kwenye meza, vilipo viatu. Mashine ikaongeza bei.
"Ni dola elfu moja na miatano"
Nikatoa
pochi yangu, nikatoa dola mia mia kumi na tano na kumkabidhi muhudumu.
Wafanyakazi wengine wakachukua viatu na kuviweka kwenye mifuko.
"Jamani kuuliza si ushamba. Hivi hiyo meza ndio inahesabu bei za vitu vinavyo wekwa juu yake?"
Nilimuuliza muhudumu baada ya kuona tukio hilo, lililo nishangaza sana.
"Ndio,
inarahisisha kazi na kutoa shida ya wateja kulalamika kwamba
tunawazidishia bei wateja. Ukiweka hapo kitu chochote kinacho uzwa humu
ndani ya duka letu, basi bei inatoka kama hapa mulivyo ona, kwahiyo
hakuna mabishano."
"Haki ya Mungu, hii mashine ikiwekwa kwenye maduka ya wachaga watafilisika"
"Wachaga wa Tanzania?"
"Ndio"
"Ahaaa kwa nini?"
"Unajua
kitu kama cha dola tano, watakuanzia kukuuzia dola kumi, ukiwa mjinga
wana kula ila ukiwa mjanja utashuka nao hadi bei halisi"
"Haaaaa, kwani wewe kaka kabila gani?"
"Ahaa kabila hapo...."
"Hapo nini si ujibu, kigugumizi cha nini?"
Phidaya alidakia kwenye mada niliyo kua nikizungumza na muhudumu.
"Mimi mwenyewe ni mchaga ila nimechanganyia na mpare"
"Mungu wangu, hayo makabila nasikia ni wabaili sana kwa nchi ya Tanzania?"
"Waongo hao, hukuna kitu kama hicho, tena ndio makabila yanayo ongoza kwa kutumia pesa bila kuijutia."
"Mmmmm"
"Usigune si unaniona mimi haoa ninavyo wapapendesha wanangu. Ngoja tuondoke kaka tumezunguka sana"
"Sawa kaka ninaitwa Salim"
"Mimi ni Eddy, huyu mke wangu na hawa ni wanangu"
"Karibuni sana"
"Asante"
Kwa
uchangamfu wa jamaa huyu, ukanifanya mwili wangu kurudi katika hali ya
kawaida hata, hasira niliyo kua nayo dhidi ya John ilanipotea. Tukatoka
nje ya duka. Tukakodisha taksi hadi Hotelini, moja kwa moja nikaingia
chumbani kwetu, nikawaacha Phidaya na wanae wakiendelea na kujipima pima
nguo na viatu walivyo nunua. Nikachukua simu iliyopo mezani,
nikaipakata mapajani, nikaingiza namba za simu ya Blanka mdogo wa
Sheila. Kwa bahati nzuri simu ikaanza kuita. Ikaita kwa muda hadi
ikakata. Nikajaribu kuipiga tena ikaita kwa muda mrefu, kabla haijakata
ikapokelewa.
"Haloo"
Nilizungumza, ila Blanka hakuitikia.
"Blanka"
"Wewe nani?"
Blanka alizungumza kwa sauti yaupole, iliyo jaa wasiwasi mkubwa.
"Upo sehemu gani?"
"Wewe nani kwanza?"
"Eddy"
"Eddy gani?"
Nikaanza kupata wasiwasi dhidi ya Blanka nikahisi nimekosea namba, kwani hata namba yenyewe sikuwa naikumbuka kivile.
"Kwani wewe upo nchi gani?"
"Tanzania,
kwani wewe ni Eddy gani au ndio hii mimamba ya Fremasoon? Hata kama
munanichukua hamuwezi kunichukja damu ya Yesu imenifunika, washenzi
nyinyi"
Simu ikakatwa nikabaki nikiwa ninashangaa, sikujua maneno yote hayo yametokea wapi.
"Labda nimekosea, ila sauti mbona niyake?"
Nilizungumza
huku nikiirudisha simu mezani nilipo itoa, nikaingia bafuni, nikaoga na
kurudi chumbani. Nikakuta simu ikimalizia kuita na kukatika. Nikafungua
kabati lenye nguo zetu, nikiwa ninaendelea kuchagua chagua nguo ya
kuvaa, simu ikaita tena. Nikaipokea na kuiweka sikioni. Huku nikisubidia
kuisiki sauti ya Blanka
"Eddy toka uje kuwaona wanao walivyo pendeza"
Haikuwa sauti ya Blanka bali ni Phidaya ndio alizungumza.
"Sawa nakuja"
Nikakata
simu, nikamaliza kuva na kutoka sebleni. Nikawakuta Shamsa na Junio
wakiwa wanapigwa pigwa picha na mama yao, kusema ukweli wamependeza
sana.
"Kaa na wewe hapo niwapige picha"
Phidaya
alizungumza, akiniomba nikae kwenye sofa walilo kaa Junio na Shamsa.
Huku akiwa ameshika camera aina ya Cannon D7 tuliyo inunua kwa ajili ya
kuchukua matukio baadhi katika siku ya kuzaliwa kwa Junio.
"Nitapigaje picha na nguo hizi?"
"Kwani zina nini, hembu kaa bwana"
"Haya mwaya mamyto"
Nikakaa katikati ya Shamsa na Junio. Phidaya akawa na kazi ya kutupiga picha huku, tukiwa tunabadilisha mikao tofauti tofauti.
"Hizi picha tunazitupia facebook"
Phidaya alizungumza huku akitufwata kwenye sofa tulilo kaa akituonyesha picha tulizo piga.
"Zimependeza"
Shamsa
alizungumza huku akiwa na furaha sana, kwani nimeamua kuifanya familia
hii kuishi kwa amani, chochote watakacho hitaji kutoka kwangu, wakipate
kwa muda muafaka.
"Haya na wewe mamyto kaa niwapige picha"
Phidaya akakaa katikati yao, na mimi nikaanza kuwapiga picha huku nao wakibadilisha miako tofauti tofauti.
"Nizamu ya baba na mama"
Shamsa alizungumza huku, akinifwata nilipo simama.
"Ile laptop mumeifungua kwenye boksi lake"
"Bado"
"Itoe"
"Ngoja nikaichukue ipo chumbani kwa Junio"
Shamsa
akaingia chumba cha Junio, akarudi akiwa na boksi lenye laptop tuliyo
nunua. Akaitoa na kuiweka mezani. Nikampa kamera, tukapiga piçha kadhaa
nikiwa na Phidaya kisha tukapiga tukiwa na mtoto wetu Junio.
"Yaani facebook leo watakoma"
"Kwànza muna account ya hiyo facebook au unasema tu watawakoma"
"Nitafungua, mimi Eddy, nifungulie kwa jina gani?"
"Mr and Mrs Eddy"
"Jina gani hilo? Mwaya Shamsa fungua kwa jina la Eddy family"
Phidaya
alipendekeza jina lake, lililo nilazimu mimi kulikubali tu kishingo
upande. Tukamaliza kupiga piga picha, nikaingia ndani kujipumzisha huku
nikiwaacha wao wakifanya shughuli zao.
***
Jioni
Phidaya akaniamsha kwa ajili ya kupata chakula cha jioni. Nikatoka na
kukuta Shamsa akichezea chezea laptop huku Junio akicheza game ya mpira
kwa kutumia deki ya 'Play station 4' niliyo mnunulia kama moja ya njia
ya kukuza kipaji chake cha kucheza mpira.
"Eddy njoo uone"
Shamsa aliniita kuangalia anacho kifanya kwenye laptop.
"Cheki hadi sasa hivi nina marafiki mia tano"
"Ahaaa mimi nilijua una kitu cha cha maana kumbe ni hao marafiki"
"Ndio wanaendelea kuniomba urafiki na kukoment kwenye picha zetu."
"Acheni munacho fanya ni muda wa msosi"
Nilizungumza huku nikiwatazama Junio na Shamsa.
"Huyo Junio wako hataki kubanduka kwenye hiyo tv na migemu yake"
"Junio, Junio"
Wala
Junio hakunisikia ninavyo muita, nikatazama jinsi anavyo wachezesha
wachezaji wa timu aliyo ichagua kwenye game hiyo. Nikamtazama mchezaji
wake anayekwenda kufunga goli, kabla hajafika golini nikachukua rimoti
ya tv na kuizima
"Dadyyyyyyyy"
"Ni muda wa kula"
"Nifainali dady"
"Eheee ni muda wa kula, utaendelea baadaye"
Ilibidi nimfokee kidogo Junio, taratibu akanyanyuka na kukaa kwenye meza ya chakula huku akiwa na sura ya kukasirika.
"Junio ukinuna unatisha"
Shamsa alimtania Junio na kumnya azidi kununa huku machozi yakimlenga lenga.
"Eddy umeniharibia mtoto"
"Kwa nini?"
"Amechukua hasira zako zote, japo ni mdogo ila kanajifanyaga kababe. Kalikua nakazi ya kupigana na wezake kule kambini"
"Kwangu atanyooka. Tena Junio ukiendea kununa, sikufanyii sherehe na vitu vyote navirudisha madukani tulipo vinunua"
"Am sorry dady"(Samahani baba)
"Nime kusamehee"
Furaha ya Junio ikarudi kama kawaida, Tukamaliza kula chakula.
"Asante dady"
"Asante Eddy na Mama"
Shamsa
na Junio wakamaliza kula na kutushukuru, kila mmoja akarudi katika
shuhuli yake. Tukasaidia na Phidaya kutoa vyombo tulivyo kula na
kuvipekeka jikoni. Uzuri wa hotel hii, unaweza kujipikia chakula chako
ukiwa unahitaji kufanya hivyo. Tukasaidiana kuviosha vyombo.
"Ehee niambie zile damu ulizitoa wapi?"
"Tutazumgumza kitandani"
"Sawa"
Tukamaliza
kuonysha vyombo na kuvipanga vizuri, tukawaaga watoto wetu na kuingia
chumbani wao wakaendelea na mambo wanayo yafanya. Phidaya akapitiliza
bafuni kuoga, baada ya muda akarudi na kujirusha kitandani.
"Nasubiria hayo mazungumzo"
Nikashusha pumzu huku nikimtazama Phidaya anaye hitaji nimuambie ni nini kilicho nikuta.
"Nina tatizo mke wangu"
"Tatizo! Tatizo gani?"
"Kipindi
fulani nilipo kua Afrika Kusini nilifanyiwa uchunguzi na kubainika nina
ugonjwa wa hasira ambao, nikikasirika sana damu puani hua zinanitoka,
pamoja na mwili kushikwa na kizungu zungu"
Nilimfinya Phidaya juu ya ugonjwa wa saratani(Canser), ambao niligundulika unaninyemelea.
"Mmmm leo ni nini kilicho kukasirisha?"
Nikamtazama Phidaya kwa macho ya kumdadisi kama anaweza kuhimili kile nitakacho kwenda kumuambia.
"Nilikumbuka, kitu licho nifanyia John. Nikajikuta nikiwa nimemasirika sana"
Ilinibidi nimdanganye tena kwani hakuwa jasira kwa lile nililo panga kumueleza kuhusiana na John
"Ni hilo tu au kuna jengine?"
"Hakuna jengine zaidi ya hilo"
"Ila baba Junio, kama ni huyo John, achana naye. Kikubwa umesha ipata furaha yako"
"Una uhakika na unalo lizungumza?"
"Kama mimi nimesha msamehe japo sihitaki kuonana naye. Kwa maana nikimuona nitatamani nimuue?"
Nikamchunguza Phidaya nikagundua ana usingizi unao mnyemelea, hata anacho kizungumza hakzingatii.
"Kwanza Junio alivyo zaliwa, aliwapeleka wapi. Hadi mukawa munazungumza na mimi?"
"Ni stori ndefu, kesho tutazungumza tukiwa tumetulia. Ila msamehe tuu"
"Siwezi kumsamehe, hadi nichukue kila kitu alicho nichukulia mikoni mwangu"
"Utavichukua vitu vipi?"
"Vingi tu"
"Mtu mwenyewe yupo huko Afrika kusini utampataje?"
"Nitampata tu"
Katikati
ya mazungumzo Phidaya akapitiwa na usingizi, mzito ulio tokàna na
uchovu wa kutwa nzima. Saa ya ukutani inaonyesha ni saa saba usiku.
Sikuwa
na hata lepe la usinguzi, nikaibeba simu ya mezana na kwenda nayo
sebleni, ambapo nikamkuta Shamsa akiwa amepitiwa na usingizi. Huku Junio
akiwa amejilaza kwenye sofa.
"Shamsa amka ukalale"
Shamsa akanyanyuka kiuvivu, akaifunga laptop.
"Niachie laptop hiyo"
"Usiku mwema"
Shamsa
alizungumza huku akipiga miyayo ya uchovu. Nikamnyua Junio na
kumuingiza chumbani kwake, huku akiwa usingizini. Nikamlaza kitandani na
kumfunika vizuri na shuka.
Nikarudi
sebleni na kukaa kwenye kiti chenye meza iliyo na laptop. Nikaifungua
na kukuta ikiwa bado ipo hewani kwenye mtandao wa Facebook. Nikatazana
tamzama alicho weka Shamsa, Picha moja niliyo piga mimi, Junio na
Phidaya inaonekana ikiwa na maoni mengi ya watu. Ikanivutia niyafungue.
Kitu kilicho nistua ni baadhi ya maoni ya watu yakionyesha masikitiko
yao juu ya kifo changu. Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi huku
wasiwasi ukinijaa. Nikataona maoni ya Blanka aliyo yaandika kwa herufi
kubwa.
'MBONA SIELEWI NI NINI HICHI?"
Nikachukua simu na kumpigia Blanka tena, safari hii akapokea haraka.
"Blanka mimi ni Eddy"
"Ndio sauti yako nimeikumbuka, jana ulivyo piga nilikua usiku nimelala"
"Vipi kuna lipi jipya?"
"Jipya bwana, ni mhabari juu ya kifo chako"
"Kifo changu, kivipi?"
"Ndio,
kitu kilicho nifanya nijue hujakufa ni picha nilizo ziona hii asubuhi
facebook, ukiwa na familia yako. Hapo ndipo nikakumbuma uliniambia
unakwenda kutafuta familia yako"
"Sasa kifo changu kipi?"
"Tumemzika majuzi juzi Eddy aliye uawa pamoja na dada Sheila"
"Fredy aneuawa?"
"Ndio, walitekwa kwenye arusi yeye na Sheila, ila hadi sasa mwili wa Sheila haujapatikana"
"Sasa nakuomba usimuambie mama kuhusiana na hii ishu."
"Eddy mama ana hali mbaya sana, amepararaizi baada ya kifo chako, hali, hanywi yupo yupo tu"
"Nini?"
"Ndio hivyo, dokta wake amesema tunaweza kumpoteza mama muda wowote kuanzia leo. Hapa nilipo nimechanganyikiwa"
Nikakata
simu, mwili mzima nikawa kama umezizima, picha ya Jonh na Sheila
zikanijia kichwani jinsi walivyo kua na furaha, nilipo waona kwenye
mgahawa.
"John nilazima ulipe kwa hili. Nikatuua kwa mkono wangu mwenyewe, ole mama yangu afe, nitakufanya kama Derick"