test

Jumanne, 1 Novemba 2016

Ridhiwani:nitahakikisha Natatua Kero Za Wananchi Kwa Wakati


Wananchi katika jimbo la Chalinze mkoani Pwani, wamekiri kuona mwanga kwa jinsi viongozi wanavyotatua matatizo yao, kufuatia kuongezeka kwa ushirikishwaji wa wananchi katika kutoa kero zao mbele za viongozi na kujadiliana utatuzi wake kwa pamoja.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa mkutano kati ya wananchi wa kitongoji cha Visakazi kata ya Ubena Chalinze na Mbunge wa Chalinze RIDHIWANI KIKWETE, ambapo sehemu kubwa ya wananchi waliohojiwa wameonyesha kukubali kwamba mikutano ya majadiliano mara kwa mara kati ya viongozi na wananchi huongeza ufanisi katika utendaji.

Naye Mbunge wa Chalinze kwa upande wake amebainisha kuwa mikutano hiyo ni sehemu ya utaratibu wa kiuongozi ambao amejiwekea katika kuhakikisha anatatua kero za wananchi wake kwa wakati muafaka na kwa kiwango kinachotakiwa.

Wakati wa mkutano huo, wananchi hao wameshukuru kwa kazi kubwa ambazo tayari zimefanyika katika jimbo hilo ikiwemo uimarishaji wa huduma za  afya, elimu na pamoja na mambo mengine ya kijamii.

“Mbunge huyu amekuja na staili kama ya wakati wa mzee wake wananchi tunapewa nafasi tunasema hata yetu binafsi naamini hii itasaidia sana na utakuwa karibu na wananchi wako", alisema Bi Semeni Masound,

Aidha  wameelezea kuridhishwa na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa katika kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Katika hatua nyingine Mbunge Ridhiwani ameshiriki katika mazishi ya Mama mzazi wa Diwani wa zamani Kata ya Bwilingu Ndg.Rashidi Shomari Lugazo.

Mbunge huyo ataendelea na ziara ya kutembelea wananchi tarehe 5 novemba.
Mwenyekiti wa Chama cha CCM Tawi la Visakazi akieleza baadhi ya malalamiko ya wananchi mbele ya  Mbunge wao Ridhiwani Kikwete hayupo pichani kwenye ofisi ya chama hicho katika mkutano.
Mbunge Ridhiwani Kikwete wa pili upande kushoto  akishiriki katika mazishi  Mama mzazi wa Diwani wa zamani Kata ya Bwilingu Ndg.Rashidi Shomari Lugazo na wa kwanza upande wa kulia ni Sheikh Hussein wa Bwilingu akitoa neno la Mawaidha katika msiba

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx