test

Jumanne, 22 Novemba 2016

KALI YA MWAKA::MWENYEKITI WA SOKO LA MBANDE AOMBA KUPIGWA RISASI MBELE YA MAKONDA


MWENYEKITI soko la Mbande Mbagala katika Halmashauri ya Manspaa ya Temeke Mukiwa Hassani hii leo ametoakaili yam waka baada ya kuomba kupigwa risasi mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda baada ya kutuhumiwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha katika upangishaji wa vizimba sokoni hapo.
  
Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kufika sokoni hapo kwaajili ya kusikilizakero zinazowakabiliwananchi ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake katika manispaa ya TEMEKE.
Unaweza ukadhani ni masihara lakini ndivyo hali halisi ilivyokuwa baada ya mkuu wa mkoa wa DSM kutoa nafasi kwa wakazi wa mbande hususani wafanyabiashara wa soko hilo kutoa kero zao.
Kufuatia tuhuma hizo ikamlazimu mkuu wa mkoa kumsimamisha mwenyekiti wa soko hilo  Hassani ili kujibu tuhuma hizo ndipo alipotoa kauli hiyo.


Kufuatia utetezi huo ikamlazimu mkuu wa mkoa kutumiabusuara ambapo akamuagiza mkuu wa wilaya ya TEMEKE kusimamia uundwaji wa uongozi wa soko hilo haraka.
Mkuu huyowa mkoa pia ametumia ziara yake hiyo kutembela eneo kitakapo jengwa kituo cha polisi katika kata ya chamazi ikiwa ni moja mikakati ya serikali katika kupambana na uhalifu.


Lengo la ziara hiyo ni kusikiliza kero za wananchi.Makonda aliytembelea Soko hilo kwa ajili ya kusikiliza hoja za wanachi hao, ambapo baadhi ya wananchi walilimlalamikia mwenyekiti wa soko hilo kuwahujumu wananchi kwa kukodisha vizimba vya kufanya biashara katika soko hilo kwa kiwango kikubwa cha fedha ilhali hatoi stakabdhi ya malipo.
Hassani aakijibu hoja hizo amedai kuwa amezushiwa na kwamba akikutwa na hatia apigwe risasi mbele ya RC Makonda 

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx