kimesaidia kuokoa zaidi ya TZS bilioni 5 ambayo ni wastani wa matumizi ya shilingi za Kitanzania milioni 110 kwa kila safari moja. Kufutia hatua hiyo, wasomi wametofautiana juu ya hilo huku baadhi wakipongeza wakati wengine wakisema kuwa kuna umuhimu wa kiongozi wa juu kama yeye kusafiri.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Mwananchi uliweza kubaini kuwa, kwa safari zote ambazo Rais Magufuli hakwenda ameweza kuokoa takribani shilingi bilioni 5.7. Fedha hizi ni makadirio ya wastani ambayo Rais na msafara wake wa watu 50 wangetumia katika safari hizo 44 ambayo kila moja ingekuwa ya siku tatu.
Mtumishi wa serikali anaposafiri kwenda nje ya nchi anatakiwa kulipwa posho shilingi 872,000 kwa siku. Kama rais angesafiri nje na wajumbe 50, jumla ya posho zao pekee kwa siku ingekuwa 43,600,000 na kama safari hiyo ingekuwa ya siku tatu gharama za posho ingekuwa shilingi 130,800,000. Kiasi hicho kikizidishwa kwa mialiko 44 ambayo Rais Magufuli hakwenda inakuwa shilingi bilioni 5.7.
Aidha, taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la Mwananchi inaeleza kuwa kuna madaraja mawili ya posho kwa mtumishi wa serikali anaposafiri kwenda nje ya nchi. Kama mtumishi anakwenda katika nchi za Bara Ulaya au Amerika ambao hawa ni daraja A, hulipwa posho ya shilingi 915,000. Kwa upande wa mtumishi anayekwenda katika nchi za Asia au Afrika ambalo hili ni daraja B, hulipwa shilingi 828, 400.
Mbali na hilo gharama nyingi za watumishi ambao huambatana na rais wangepewa fedha za suti, fedha za kujikimu na usafiri wa ndani ya nchi atakapokuwa na posho yake huongezeka kama atakuwa angani kwa zaidi ya saa nne wakati wa safari.
Source:- Mwananchi Blog