Baada ya vyombo vingi vya habari kuripoti taarifa Ya Mchezaji wa timu ya Sonderjyske na Mshambuliaji wa Timu ya taifa ya Uganda Emmanuel Okwi Taarifa ambazo KwataUnit.com tumezipata kupitia mtandao wa airtelfootball.ug zinasema kuwa Okwi amekanusha kufanya mazungumzo Ya Kujiunga na Simba.
Okwi amesema "Siyo kweli, mimi mwenyewe nimesikia hizo taarifa, akaongeza kwa kusema Hakuna makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa na siko katika mazungumzo na Simba. "
Okwi mpaka sasa ameshacheza mara 4 pekee katika klabu yake ya sasa ya huko nchini DenMark toka alipoondoka Simba na kujiunga nayo.