Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli, jana tarehe
19 Novemba, 2016 amemtembelea na kumjulia hali Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Bw. Martin Shigella ambaye amelazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Bw. Martin Shigella alifikishwa hospitalini hapo tangu Jumatano iliyopita kwa ajili ya kupata matibabu.
Akimpa pole wodini humo Rais Magufuli alisema “Nakupa
pole sana Ndg. Martin Shigella kwa maradhi yaliyokupata, nakuombea kwa
Mwenyezi Mungu upone haraka na urejee katika kituo chako cha kazi ili
uendelee na majukumu ya ujenzi wa Taifa”
Hali ya Bw. Martin Shigella inaendelea vizuri.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam