Rais wa China Xi Jinping, na rais mteule wa marekani , Donald Trump wamekubaliana kwa njia ya simu kukutana katika siku za hivi karibuni ili kujadiliana kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Runinga ya China imemnukuu bwana Xi akimwambia bwana Trump kwamba ushikamano ndio chaguo la kipekee katika uhusiano wao.
Katika kampeini yake bwana Trump amekuwa akiilaumu China kwa kufanya biashara haramu na udanganyifu wa fedha.
Pia ameonya kuwekeza asilimia 45 ya ushuru kwa bidhaa zinazotoka nje ya china.
Ofisi ya bwana trump imesema viogozi hao wawili wameonyesha heshima katika mazungumzo yao kwa njia ya simu