Hali
hiyo imetokea baada ya Aunty kuweka picha ya kumtakia siku njema ya
kuzaliwa rafiki na msanii mwenzake, Maimartha Jesse kwa kuandika, “Happy
bday Kipenzi cha Roho yangu …..Unajua kama Nakupenda cha zaidi Naomba
Yesu Akutunze milele.”
Katika
post hiyo, followers kadhaa wa Aunty walikomenti akiwemo staa mwenzake
kwenye tasnia hiyo, Wema Sepetu aliyekomenti “Yesu atamtunza…” Baada ya
hapo, Aunty akaibuka na kumtolea povu Wema akimchana “Achana na mm ww
@wemasepetu“ hali iliyoibua maswali na mijadala mingi mitandaoni, huku
watu wakitaka kujua kwa nini Aunty amemshushua hivyo Wema.
Chanzo
ni Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, Wema kumsema vibaya Aunty kwenye
mitandao ya kijamii hasa Instagram, Kwa hali ilivyofikia mpaka sasa
inaonesha sio rahisi tena kwa waigizaji hao kuelewana.
Tangu
siku za hivi karibuni, Wema alipokosana na rafiki yake Muna Love na
kumsema vibaya kwa kutumia video aliyojirekodi na kuisambaza mitandaoni,
Wema kwa sasa amekuwa akijitahidi kuwa karibu na Aunty ili warudishe
urafiki wao wa zamani japokuwa jitihada zake zinaonesha kugonga mwamba
baada kuambulia maneno mazito kutoka kwa Mama Cookie.
Post ya Mama Cookie.