test

Jumatano, 12 Oktoba 2016

VIDEO:Mwalimu atekwa na kudungwa sindano za sumu,Mkurugenzi wa Arusha ahusishwa


Mwalimu wa Shule ya Msingi Unga Limited iliyoko kata ya Unga limited Mkoani Arusha anayefahamika kwa jina la Batuli Hamadi alitekwa na watu wasiojulikana na kusadikika kuwa alichomwa sindano za sumu.

   Akielezea tukio hilo Batuli anasema,mnamo tarehe tatu mwezi huu wa kumi muda wa saa tatu usiku alitoka nyumbani kwake na kuelekea dukani ili kununua vocha ili aweke kwenye simu.Lakini ghafla akiwa njiani akirudi nyumbani toka dukani alitekwa na watu wasiojulikana na kupandishwa kwenye gari na kupelekwa sehemu isiyojulikana na kufanyiwa matukio ya ajabu na yeye mwenyewe anasema mara ya mwisho alifumbwa puani na mmoja wa watekaji na ghafla akapoteza fahamu.
 Tukio hili linamhusisha Mkurugenzi wa Arusha moja kwa moja kama yeye mwenyewe anavyosimulia.Msikilize hapa chini.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx