test

Jumapili, 2 Oktoba 2016

VIDEO:Hii ndiyo show kabambe ya Amphibious Landing ya JWTZ mbele ya JPM


JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limehitimisha maadhimisho ya miaka 52 ya kuasisiwa kwa jeshi hilo, kwa kuonesha zoezi la medani liitwalo ‘Amphibious Landing’ lililofanyika Bagamoyo, Pwani.

Tukio hilo lililokuwa na mvuto wa aina yake, lilifanywa juzi jioni katika kijiji cha Baatini huku likishuhudiwa na Rais John Magufuli, Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Abdulhamid Yahaya Mzee.
Katika mazoezi hayo ya wiki mbili, Jeshi lilionesha uhalisia, jinsi wanavyoweza kukomboa eneo lililotekwa.
Wakati wa zoezi hilo, Meja Patrick Sawala alikuwa akielezea mtiririko wa matukio kwa Rais Magufuli na baada ya vikosi kumaliza kazi ya kukomboa eneo lililotekwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali, Davis Mwamunyange alisema anajivunia kuwa kiongozi wa chombo hicho.
‘Najivunia kuwa kiongozi wa chombo hiki, kwa sababu nina askari na maofisa wazuri, wanaojituma sana, weledi, wazalendo na wako tayari kulinda watanzania na wanafanya hivyo kwa maslahi ya nchi yao, na hata nje ya nchi tunajivunia kwa sifa yetu ya nidhamu na uimara wetu,” alisema Mwamunyange.
Mwamunyange alimwambia Rais Magufuli kuwa vifaa hivyo vya kijeshi ni mali ya watanzania, vimenunuliwa na watanzania na vyote vinaendeshwa na watanzania wenye maadili na weledi na nidhamu ya hali ya juu kwa nchi yao.
Katika mazoezi hayo, jeshi lilitumia ndegevita, vifaru vyenye uwezo wa kukaa baharini na kutembea nchi kavu, melivita, boti za kasi.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx