Moja kati ya story zilizo kiki kinoma hapo jana ni ile ya Diamond Platnumz kufungua milango kwa wasanii wote wenye vipaji na wenye malengo ya kufika mbali kupitia kazi yao ya muziki kujiunga na lebo ya WCB Wasafi.
Alivitaja vigezo ambavyo msanii anatakiwa kuwa navyo ili aweze kupata nafasi ya kusainiwa katika lebo yake, na akasema kwamba kwasasa lebo hiyo haiko tayari kuwasainisha wasanii wanaotoka nje ya Afrika Mashariki na wale ambao ndio wanaanza katika kazi ya muziki (Underground) na badala yake akadai bado anajikita katika kuwafikisha mbali zaidi wasanii wake ambao amewakuza yeye Harmonize na Raymond.
Sasa leo ameamua kubonga na ma-underground na kuwapa maneno kuntu kama ushauri na endapo wakiuchukua na kuufanyia kazi huenda wakafika mbali.
“Cha kwanza naomba niwaambie watoe zile dhana kwamba ili ufanikiwe ni lazima ufanye ushirikina au uchawi, huwezi kufanikiwa. Ni lazima ufanya kazi kwa bidii, uangalie ni fursa ipi ambayo wasanii wengine hawaifanyi wewe upite nayo. Jitahidi kuwa muandishi mzuri kwasababu soko la Tanzania linataka uandishi mzuri, imba vizuri fanya mazoezi, kuwa na nidhamu, ishi na watu vizuri, ipeleke nyimbo sehemu husika au tafuta management bora naamini ipo siku mwenyezi mungu atakufikisha.”