Siku
moja baada ya matokeo ya darasa la saba kutangazwa, baadhi ya wamiliki
wa shule wamelijia juu Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kwa kufuta
matokeo ya wanafunzi wao, huku mmoja wao akibubujikwa na machozi akidai
wamehujumiwa.
Ikitangaza
matokeo hayo juzi, Necta ilisema imefuta matokeo ya wanafunzi 238 kwa
sababu ya udanganyifu, ikiwatuhumu wakuu wa shule sita na walimu
kuhusika kuiba mitihani, kuwapa majibu watahiniwa au kuwafanyia mtihani.
Necta
ilienda mbali zaidi na kudai kuwa kwenye shule moja, walimu walijificha
bwenini, chooni na ofisini ambako wanafunzi waliwafuata na kupewa
majibu na baadaye kuyasambaza kwa wenzao.
Lakini,
walimu hao wamepinga vikali tuhuma hizo za kushiriki katika
udanganyifu, isipokuwa shule moja tu ambayo ilisema mwalimu aliyehusika
ameshachukuliwa hatua.
“Sijafurahishwa na kitendo cha Necta kuifutia matokeo shule yetu. Hiyo ni hujumu,” alisema mmiliki wa shule ya msingi Tumaini iliyopo Sengerema mkoani Mwanza, Kandumula Maunde.
Huku akilia, Maunde alisema wakati tukio hilo lilotokea saa 5:00 asubuhi, hakuwepo na hakushirikishwa.
“Niliitwa
kesho yake na kupata maelezo kuwa wanafunzi wa shule yako wamekamatwa
kwa sababu wameandikiwa majibu ya mtihani kwenye sketi, sikukubaliana
nao,” alisema.
Kwa
mujibu wa Necta, mmiliki huyo aliiba na kuandaa majibu ambayo
watahiniwa wake waliandika kwenye sare za shule na kuyatumia ndani ya
chumba cha mtihani.
Necta
imewataja waliohusika kuwa ni mmiliki aliyetajwa kwa jina la Jafari
Maunde, msimamizi anayeitwa Alex Kasiano Singoye na wanafunzi wote.
Alisema hakukubaliana na kitendo hicho kwa sababu wanafunzi hao walikuwa wameandaliwa vizuri kujibu mitihani yao.
Maunde
aliliomba baraza la mitihani kupitia upya uamuzi wake wa kuifutia shule
hiyo matokeo kwa kuwa umeathiri maisha ya wanafunzi waliokuwa na ndoto
za kuendelea na masomo.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule hiyo waliofutiwa matokeo waliiomba Necta
kuangalia upya uamuzi huo. Wanafunzi hao walieleza kuwa msimamizi wa
mtihani wa siku hiyo alikuwa akiwasumbua na aliwalazimisha waandike
maelezo ya kukiri kuwa walikamatwa na majibu.
“Msimamizi
alitulazimisha tuandike kwenye ubao baada ya kumaliza mitihani maelezo
yakisema tumekamatwa na majibu ya mtihani yakiwa yameandikwa kwenye
sketi tulizokuwa tumevaa,” alisema mmoja wa wanafunzi hao, Kefa Matini.
Kwa
upande wa shule ya msingi ya Little Flower iliyopo Serengeti mkoani
Mara, walimu walisema uamuzi wa kufutiwa matokeo ni adhabu isiyostahili.
Wanafunzi 37 wa shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki, Parokia ya Magumu wamefutiwa matokeo.
Necta imeeleza kuwa mwalimu mkuu wa Little Flowers aliiba mtihani, kuandaa majibu na kumpa msimamizi mkuu pamoja na wasimamizi wengine ili wawape watahiniwa.
Necta imeeleza kuwa mwalimu mkuu wa Little Flowers aliiba mtihani, kuandaa majibu na kumpa msimamizi mkuu pamoja na wasimamizi wengine ili wawape watahiniwa.
Imesema
waliohusika ni mwalimu mkuu anayeitwa Cecilia Nyamoronga, msimamizi
mkuu (mwalimu), Haruni Mumwi na msimamizi (mwalimu), Genipha Simon na
watahiniwa wote.
Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Paskael Chacha alisema uamuzi huo umewaumiza walimu na watoto waliofanya mtihani walioko shuleni na wazazi kwa kuwa hawajapewa sababu za udanganyifu huo na ulimhusisha nani na lini.
Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Paskael Chacha alisema uamuzi huo umewaumiza walimu na watoto waliofanya mtihani walioko shuleni na wazazi kwa kuwa hawajapewa sababu za udanganyifu huo na ulimhusisha nani na lini.
“Walimu
hawakuwepo shuleni, mkuu wa shule ndiye alikuwa akiruhusiwa kuwepo
shuleni kwa muda mfupi. Inanipa shida kujua udanganyifu ulifanyikaje na
ulimhusisha nani.
"Hili
suala linatupa shida kwa kuwa wasimamizi walioletwa siku ya kwanza si
waliofika kusimamia. Sasa taarifa kama hizi zinauma sana,” alisema.
Alipotakiwa
kutoa ufafanuzi wa taarifa zinazodai kuwa siku ya mtihani mtoto mmoja
alikamatwa na karatasi ya majibu na kumtaja mkuu wa shule kuwa ndiye
aliyempa, mwalimu huyo alikana na kudai kuwa hana taarifa.
Majibu ya Dr. Msonde
Akizungumzia
malalamiko hayo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema
wanaosema wameonewa wanatakiwa kuomba radhi na kukubali adhabu kwa
sababu waliokamatwa walikutwa na uthibitisho, akitoa mfano wa Shule ya
Msingi Tumaini.
Kwa
upande wa Shule ya Msingi Little Flower, Dk Msonde alisema ofisa wa
baraza la mitihani alishuhudia mwalimu akipitisha karatasi ya majibu kwa
wanafunzi .
“Sasa
hapo utasema umeonewa? “Tumezoea kuona (matukio ya udanganyifu) yale ya
mwanafunzi mmoja, lakini haya yanatisha. Mwalimu au msimamizi
anamsaidia mwanafunzi, hii si sawa,” alisema.