- Matokeo yanaonyesha IMANI kubwa ambayo wananchi wanayo kwa Rais Magufuli. Hata hivyo IMANI hiyo inakuja na wajibu mkubwa sana na Rais asitumie vibaya imani hiyo. Kiongozi mwenye busara hawezi kutumia imani hii kwa kukandamiza demokrasia na kukanyaga Katiba.
- Matokeo pia yanaonyesha kuwa Wabunge na Madiwani kwa kiasi kikubwa wana IMANI ya wananchi wao wanaowawakilisha. Huu ni wajibu na fursa kwa Wabunge wa Upinzani kuonyesha uongozi mahiri wenye kutoa majawabu ya changamoto za wananchi kwenye maeneo yanayoongozwa na Vyama vya Upinzani.
Tujifunze kukubali tusiyopenda kuyasikia. Wakati tunapambana vita adhimu sana dhidi ya Udikteta Mamboleo unaonyemelea nchi yetu, pia kwa nguvu hizo hizo tuonyeshe tofauti ya kiuongozi katika Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji tunayoongoza
By Zitto Kabwe