Ubuyu
unaotrendi Bongo unamgusa staa wa Bongo Fleva anayekamata anga za
kimataifa, Vanessa Mdee ‘V-Money’ ambaye wikiendi iliyopita alitawala
mitandao ya kijamii kwa picha yake iliyomuonesha akiwa amevaa kibukta na
kuachia maungo yake wazi kisha mashabiki wakahoji kuwa rangi ya maungo
haifanani na rangi ya uso wake ‘eti baadhi ya sehemu amekunywa maji
mengi’. Mwana-ubuyu wetu alipoona picha hiyo imefunika mitandaoni,
aliamua kuangaza kwenye kila akaunti ambapo alikutana na komenti nyingi
zilizoonesha madai kuwa mwanadada huyo, kuna wakati huwa anaediti sura
yake na kuonekana mweupe na kuna wakati anakuwa na ngozi ya maji ya
kunde. Hata hivyo, wapo waliomvaa jumlajumla wakidai amekuwa akitumia
mkorogo na kusahau baadhi ya maungo lakini pia wapo waliodai kuwa ni
picha za Instagram ambazo mtu ana uwezo wa kuzifanya zikang’aa na
akaonekana apendavyo.
“Picha
za mtandaoni ni noma! Unaweza ukadhani kitu kimetoka Ulaya leoleo
lakini ukikutana nacho laivu, utajiuliza mara mbilimbili. Hicho ndicho
kinachotokea kwa akina dada walio wengi wanaopenda kuuza sura,” alisema
Antonio, mmoja wa wachangiaji mtandaoni. Baada ya Wikienda kuona ishu ya
Vanessa imekuwa gumzo kutokana na komenti hizo ndipo likajiongeza na
kuufanyia kazi ubuyu huo kwa kutafuta ukweli kwani mbali na rangi ya
ngozi, pia wapo waliomdisi kimavazi lakini pia wapo waliompongeza kwa
kwenda na wakati wakidai kuwa anavaa kimataifa zaidi. Wikienda kama
kawaida yake lilimsaka Vanessa ili kumfikishia tuhuma zake za kujiediti
na kutumia mkorogo.
VANESSA ATOKWA POVU
Katika
kumtafuta Vanessa ili kuzungumzia kile kilichotrendi mtandaoni,
Wikienda lilimwendea hewani kupitia simu yake ya mkononi kwani hakuwepo
Dar badala yake ilielezwa kwamba yupo nchini Kenya akirekodi na
mwanamuziki mkubwa wa Marekani, Trey Songz. Intavyu ya Vanessa na
Wikienda ilikuwa hivi; Wikienda: Vanessa mambo vipi? Kuna maswali kadhaa
nataka kukuuliza, uko free tuchati? Vanessa: Oke.
Wikienda:
Kuna picha zipo mtandaoni umebebwa stejini, mashabiki wako wanasema
make-up zinakusaidia na wengine wanadai unajichubua usoni tu, mwilini
umeusahau! Je, wewe unaliongeleaje hilo? Vanessa: Unadhani swali lako
linanijenga nini mimi? Nakuomba uchunguze maswali yako kabla ya
kuniuliza.
Wikienda:
Swali lina maana kubwa, wewe ni kioo cha jamii, kwa kuwekwa mtandaoni
na kujadiliwa kuwa unajichubua, huoni kama unachafuliwa? Kwangu mimi
nimeona nikupe nafasi ya kufunguka huenda kuna watu wanataka
kukuharibia.
Vannesa:
Kwa sasa niko Kenya, nafanya kazi na msanii mkubwa wa Kimarekani, Trey
Songz hujaandika lakini unataka kuniuliza maswali ya ajabu tu, kweli
hayo ni maendeleo? Wikienda: Kazi yangu ni kuuliza kila kitu kama
nakiona hakiendi sawa hasa kwa mastaa kutokana na gazeti
ninaloliandikia, wewe jibu tu kwani nimekupa nafasi. Vannesa:
Umenikwaza, naomba tuachane kwa sasa! Baada ya kuachana na Vanessa,
kumbe alimpatia meneja wake namba ya mwandishi wetu ambaye alimtafuta
Mwana-ubuyu kwa ajili ya kuweka mambo sawa ambapo naye alifunguka kama
hivi.
Meneja:
Naitwa Tommy kwa jina. Ni meneja wa Vanessa, naomba tuwasiliane
tafadhali. Wikienda: Poa una jipya lipi? Naona mmepaniki mpaka wewe
umenipigia. Meneja: Yaah! Nimeona maswali unayomuuliza Vannesa, naona
kama unauliza kabla ya kuchunguza nadhani kazi yako inakutaka kuwa
makini kwanza. Wikienda: Mimi niko makini sana ila ninyi mmepaniki, staa
hatakiwi kupaniki, anatakiwa kujibu kile anachoulizwa tu.
Meneja:
Oke! Mimi ndiye msemaji wa mwisho wa Vanessa, niulize nitakujibu.
Wikienda: Kuna madai kuwa msanii wako anajichubua kwa sababu kuna picha
imetrendi akiwa stejini na mwanaume, maungo yake yanaonekana kuwa meusi
wakati usoni ni mweupe, je, unaweza kulijibu hilo?
Meneja:
Kwanza nikurekebishe, yule mwanaume ni Jux, lakini Vanessa hajichubui,
anaipenda ngozi yake na nikwambie tu kwenye ulimwengu wa kisasa, Smat
Phones zinatofautiana na inawezekana picha zinakuwa na ubora tofauti
kutokana na kamera za simu kwani utakuta huyu anatumia Tecno, mwingine
anatumia Iphone, lazima ubora wake utakuwa tofauti. “Tunaona kila kitu
kinachoandikwa mtandaoni na siyo kila action inatakiwa kuwa na
reaction.
Sometimes
ukikaa kimya pia nalo nijibu. Wewe unajua tupo kwenye karne gani. Smart
phones ni nyingi na kila simu ina uwezo wa kamera yake. “Huwezi kumzuia
shabiki, hata akiwa na aina yoyote ya simu, akitaka kupiga picha na
Vanessa, nitaruhusu tu. “Kwa hiyo, quality ya picha iliopigwa na kamera
ya shabiki wa Vanessa haikuwa sawa na wala siyo kwamba anajichubua,”
alifunguka meneja huyo.
Alimalizia: “Vanessa anapenda ngozi yake na hana sababu ya kujichubua. She is comfortable in her skin aliyozaliwa nayo.”
NENO LA MHARIRI
Ubuyu
unampongeza Vanessa kwa kuwa mvumilivu kwani maneno yaliyowekwa
mtandaoni yanataka moyo, lakini ili uwe staa unatakiwa kukubaliana na
kila linalotokea kwani kuna watakaokukubali na watakaokukataa. Lengo la
kuandika Ubuyu huu ni kumpa nafasi ya kufungukia suala la mkorogo kwani
si zuri na kumkubusha kama anatumia, basi aache kwa ajili ya afya yake.
Ikumbukwe tu kuwa ubuyu hauna lengo la kumkandamiza staa yeyote bali ni
kumrekebisha pale anapokosea na anapotofautiana na shabiki wake kuwekwa
sawa kwani ndiyo kazi ya kolamu hii.