test

Jumapili, 25 Septemba 2016

Trump kiboko: Atishia kumualika mpenzi wa zamani wa Clinton kwenye mjadala kesho


Donald Trump ametishia kumualika mwanamke ambaye alikuwa mpenzi wa Bill Clinton akiwa kwenye ndoa na Hillary Clinton.

Trump amesema atamualika Gennifer Flowers akae mbele kabisa, kwenye mjadala baina yake Trump na mpinzani wake wa kugombea urais, Hillary Clinton, hapo kesho.
Bwana Trump alisema hayo, kujibu matamshi ya bilionea anayeshindana naye, Mark Cuban ambaye alisema, kampeni ya Clinton imempa kiti cha mbele katika mjadala huo.
Gennifer Flowers, mrembo wa zamani, amejibu kwenye Twitter, kwamba amepokea mualiko wa Bwana Trump.
Haijulikani kama Trump atafuata tishio lake hilo au la.
Gennifer Flowers

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx