test

Jumapili, 25 Septemba 2016

Prof. Lipumba aanza kazi hivi leo kwa kishindo


BAADHI ya mali za Chama cha Wananchi (CUF) hazijulikani zilipo na tayari Prof. Ibrahim Lipumba ameanza kuzisaka.
Taarifa kutoka kwa chanzo chetu ndani ya CUF zinaeleza kuwa, miongoni mwa mali hizo ni magari matano ya chama hicho.
Taarifa zaidi zinaeleza, kabla ya Prof. Lipumba kuingia Ofisi Kuu ya chama hicho zilizopo Buguruni jijini Dar es Salaam jana mchana, magari hayo yalikuwa tayari yameondolewa.

Na kwamba, juhudi za kutaka kujua magari hayo mahala yalipo zimeanza kuchukuliwa kwa Prof. Lipumba kuwasiliana na baadhi ya viongozi waliokuwa na dhamana na ofisi hiyo kabla ya jana.
“Magari kama sita hayapo ndani ya ofisi hizo, Prof. Lipumba ameanza kuuliza magari hayo yapo wapi?,” kimeeleza chanzo hicho na kuongeza;
“Alimpigia Mtatiro (Julius Mtatiro-Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la CUF) lakini alisema hajui, akampigia Paku (Abdalla Paku-Ofisa Utawala wa CUF) alikata simu na alimpigia Bashange (Joram Bashange Mkurugenzi wa Fedha wa CUF) alimjibu kuwa yupo mkoani.”
Hata hivyo, mtandao huu umemtafuta Abdul Kambaya anayetajwa kuwa mtu wa karibu na Prof. Lipumba ambaye amethibitisha taarifa hizo.
“Ni kweli magari hayapo na Profesa amekuwa akifanya juhudi za kutaka kujua magari hayo yalipo.
“Bado hatujaangalia mambo mengine zaidi lakini kuna baadhi ya vitu havipo na tutaendelea kuangalia mali ipi ya chama na nani anayo,” amesema Kambaya na kuongeza;
“Mali za CUF ni za wanachama wote na hakuna shaka tutajua zilipo. Hatuamini kama zimetoka nje kwa njia za hovyo ila naamini mwenyekiti anataka kujua tu mali hizo zipo wapi kwa kuwa anawajibuka kujua.”
Kambaya amebainishwa kwamba, Prof. Lipumba amekuwa akiwasiliana na baadhi ya viongozi ili kutaka kujua yalipo magari hayo.
“Sijui kwa watu wengine lakini najua kuwa amewasiliana na Bashange ambaye alijibu kwamba yupo nje ya Dar es Salaam,” amesema Kambaya

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx