test

Ijumaa, 23 Septemba 2016

Tathmini ya kiwango cha uharibifu wa mazingira kilichosababishwa na tetemeko la radhi zaanza kufanyika





maxresdefault-1
Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia Muungano na Mazingira imeanza kufanya tathmini ya kiwango cha uharibifu wa mazingira kilichosababishwa na tetemeko la radhi lililotokea Mkoani Kagera hivi karibuni na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa miundombinu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa wizara hiyo January Makamba, alipombelea waathirika wa Tetemeko hilo akiwa na wataalam kutoka Baraza la taifa la hifadhi ya mazingira (NEMC), ambapo amesema watachunguza mfumo wa mazingira ulivyoathirika, ili kujiridhisha kama kuna uharibifu wa mazingira unaoweza kujitokeza baada ya  kufanyika kwa ukarabati mpya.
Amesema wizara yake imetoa wataalam kadhaa watakaotafiti namna vyanzo vya maji vilivyoathrika,ikiwemo mifumo ya maji safi na taka ili kuzuia uwezekano wa kutokea mlipuko wa magonjwa yanayoweza kutokea kutokana na miundombinu mingi kuaribika wakati wa tetemeko hilo.
Pamoja na Makamba kutetembea majeruhi katika hospitali ya Mkoa Kagera na waathirika katika wilaya za Missenyi na Manispaa ya Bukoba,baadhi ya waathrika wanalalamikia kuchelewa kwa misaada na kuomba kasi ya ugawaji kuongezwa.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx