Majirani wakiwa katika hekaheka ya kumaliza ugomvi.
Mama wawili waliofahamika kwa majina ya Mama Idrisa na Mama Yusuf wakazi wa Baa-Mbili, Mtongani jijini Dar wakiwa wamekunjana.
Chanzo makini kilichoshuhudia timbwili hilo mwanzo-mwisho na kufanikiwa kupata picha kiliweka wazi kuwa, lilitokea wiki iliyopita huku chanzo kikiwa ni ugomvi wa watoto wa wazazi hao.“Ilikuwa ni kama sinema ya bure kwani mama Idrisa na mama Yusuf walianza kupigana kama utani lakini baadaye wakajikuta wakivuana mpaka nguo kisa ugomvi tu wa watoto jamani, hii ni kali ya mwaka,” alisema shuhuda huyo na kuongeza:
“Walifunga mtaa na mbaya zaidi watoto walikuwa wakishuhudia ngumi hizo ambazo wapiganaji ilifika wakati wakawa watupu, ilikuwa aibu sana kwa kweli.”
Baada ya ubuyu huo ulioambatana na picha kutua kwenye meza ya dawati hili, mwandishi wetu alifunga safari hadi eneo la tukio na kufanikiwa kuzungumza na mama Idrisa ambaye aliamua kufunguka kilichosababisha ugomvi huo.
“Muda huo mama Yusuf alikuwa ameshafika eneo hilo, akampiga Idrisa akidai anarudishia kama alivyompiga mwanaye, hali ile iliniuma sana.
“Ikabidi nimuulize kwa nini anafanya hivyo wakati aliwahi kusema ugomvi wa watoto hawezi kuingilia? Hakunijibu badala yake alianza kuniporomoshea matusi mazito.“Mimi niliendelea na shughuli zangu huku akiendelea kunitukana mpaka majirani wengine wakawa wanajiuliza anayetukanwa ni nani maana nilikuwa kimya, mwishoni nikamfuata kama mdogo wangu ili tuyamalize lakini alinipiga kofi la nguvu.
“Kutokana na maumivu niliyoyapata nikashindwa kuvumilia, nikamrudishia na hapo ndipo tukashikana mpaka nguo zikatuvuka maana nilikuwa nimevaa blauzi tu na kitenge tukabaki watupu, kiukweli nisingependa haya mambo yawekwe kwenye vyombo vya habari maana ni aibu na ndiyo maana sijaenda polisi wala kwa mjumbe,” alisema mama Idrisa.
Mama Yusuf hakuweza kupatikana baada ya paparazi wetu kufika nyumbani kwake na kuambiwa ameenda kliniki.
Naye mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la mama Iddi alisema hana taarifa za tukio hilo na kwamba wanaoweza kulizungumzia ni wahusika.