Serikali mkoa wa Singida, imepiga marufuku matumizi ya madawati ya shule za msingi na sekondari kwenye mambo yasiyo ya elimu, ikiwemo mikutano na sherehe mbalimbali za kijamii.
Mkuu wa mkoa wa Singida, mhandisi Mathew Mtigumwe ametoa agizo hilo juzi, wakati akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya madawati 144 kati ya 335, yaliyotolewa msaada na kampuni ya Tigo Tanzania.
Alisema madawati katika shule zote za msingi na sekondari yanapaswa kutunzwa vizuri, ili yaweze kutumika kwa mda mrefu zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Singida,mhandisi Mathew Mtingmwe,Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa madawati 335 yenye thamani ya zaidi ya shilingi 56 milioni yaliyotolewa msaada na kampuni ya TIGO jana.Mhandisi Mtigumwe,ameagiza madawati hayo yatunzwe ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.Kulia ni meneja wa kanda ya Singida,Dodoma na Kondo kampuni ya TIGO,Aidan Komba na mkurugenzi wa kanda kaskazini,kampuni ya TIGO,George Lugata.
“Madawati haya yanagharimu fedha nyingi kuyatengeneza yasipotunzwa vizuri,yataharibika mapema. Kwa hiyo nasisistiza yasimamiwe na kutunzwa vizuri na yafanyiwe ukarabati mapema pindi yanapoharibika,” alisema mkuu huyo wa mkoa.
Aidha, mhandisi Mtigume alitumia fursa hiyo kuipongeza na kuishukuru kampuni ya Tigo Tanzania, kwa ushirikiano wake na serikali ya mkoa, katika kutoa huduma za msingi wa wananchi wa mkoa wa Singida.
Awali mkurugenzi wa Tigo Tanzania KANDA YA kaskazini George Lugata, alisema madawati hayo yatasambazwa kwenye shule za msingi tano za halmashauri ya wilaya ya manyoni, manispaa ya Singida na halimashauri ya wilaya ya Singida.
“Msaada huu wa madawati ni sehemu ya kuunga mkono juhudu za serikali ya awamu ya tano,chini ya Rais Dk. Magufuli za elimu bure. Tigo Tanzania itahakikisha shule zimekuwa na madawati ya kutosha na kwamba tatizo la madawiti linaisha nchini,” alisema.
Akisisitiza, alisema tafiti nyingi zimeonyesha kuwa mazingira ya kufundishia na kujifunzia yakiboreshwa, yana mchango mkubwa katika ufaulu wanafunzi.
“Hivyo basi, huu ndio msingi wa maamuzi yetu ya kuchangia madawati 335 yenye thamani za shilingi 56 milioni kwa shule tano za msingi tano mkoni Singida,” alisema mkurugenzi Lugata.