test

Jumatano, 14 Septemba 2016

ASALI: TIBA YA UNENE UNAOWAKERA WANAWAKE


Karibuni tena katika sehemu hii ya makala yetu ya leo kuhusu kupunguza unene, mada ambayo imeonekana kuvuta hisia za wasomaji wengi. Tatizo la unene limekuwa sugu. Kila mmoja anajaribu kutafuta suluhisho la tatizo hilo.

KANUNI ZA KUPUNGUZA UZITO
Kanuni ya kwanza ya kupunguza uzito inatueleza kuwa ili mtu upunguze uzito, unahitaji kutoa kalori nyingi mwilini na kuingiza kalori kidogo (Less Calories In + More Calories Out= Weight Loss). Kwa lugha nyepesi, unapokula chakula chochote unaingiza kalori mwilini na unapofanya mazoezi au kazi yoyote unatoa kalori mwilini.



Hivyo kupunguza unene ni lazima ujinyime kula ili uingize kalori kidogo lakini ufanye sana kazi au mazoezi ili utoe kalori nyingi mwilini. Baadhi ya watu wamesema kuwa wanajinyima kula lakini hawapungui. Kujinyima kula peke yake hakutoshi kama hufanyi kazi au mazoezi yoyote ya kutoa kalori nyingi kuliko unazoziingiza mwilini mwako.
ASALI KATIKA KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE
Baada ya kuzingatia kanuni hiyo, hatua inayofuata ni matumizi ya asali kwa mpangilio maalum unaoweza kukusaidia kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka, wakati ukifanya mzoezi na kujinyima kula.

Matumizi ya asali ni rahisi sana. Kwanza kabisa hakikisha unapata asali halisi mbichi na siyo asali feki. Mjini kuna baadhi ya watu hutengeneza vitu mfano wa asali, matumizi ya asali hiyo hayawezi kukusaidia zaidi ya kukuletea matatizo mengine ya kiafya.

Kuna kampuni na maduka (kama super markets) zinazouza asali halisi, nunua asali mbichi kutoka sehemu inayoaminika. Kula vijiko viwili (vya chai) vya asali kila siku wakati wa kwenda kulala. Katika muda wa saa nne za mwanzo za usingizi, asali itayeyusha mafuta (fat) mengi mwilini sawa na kufanya mazoezi makali.

Mwanzilishi wa dayati hii ni Mike McInnes ambaye yeye ni raia wa Scottland na kitaaluma ni Mfamasia. Mtaalamu huyu aligundua kwamba wanariadha ambao hula matunda yenye virutubisho vingi vya ‘fructose’ (kama vile matunda yaliyokaushwa na asali) hupunguza mafuta mengi mwilini na huwa na stamina nyingi.

Ili kufaidi vizuri manufaa ya asali katika kukusaidia kupunguza unene na mwili kuupa nguvu, ni vizuri ukatumia asali hiyo kama ilivyoelezwa hapo juu huku ukifanya mazoezi ya viungo, angalau mara tatu kwa wiki.

Ni lazima ieleweke kwamba vitu vitatu lazima vifanyike kwa pamoja ili kupunguza unene kama unavyokusudia. Kitu cha kwanza ni kula vyakula sahihi na kwa kiasi kidogo, pili kula asali halisi na mbichi kila siku kabla ya kulala na tatu kufanya mazoezi au kazi nzito ili kutoa kalori mwilini. Umuhimu wa asali hapa ni ule uwezo wake wa kuyeyusha mafuta mwilini kwa haraka ukiwa umelala na wakati huo huo kuupa mwili stamina.

ASALI NA MDALASINI
Mchanganyiko mwingine ambao umeelezwa kusaidia sana kupunguza uzito, ni asali na unga wa mdalasini. Mchanganyiko huu ni kama kinywaji ambapo utatakiwa kuchanganya asali, abdalasini na maji moto kisha kunywa mara mbili kwa siku.

Ili kupata mchangayiko unaotakiwa, chukua nusu kijiko cha unga wa adbalasini (kijiko kidogo cha chai) kijiko kimoja cha asali (saizi ya kijiko cha chai) na kikombe kimoja cha maji yaliyochemka.

Anza kuchanganya maji moto na unga wa abdalasini, koroga hadi uchanganyike vizuri kisha funika na uache muda wa nusu saa ili maji yapoe. Baada ya maji kupoa, weka asali yako kijiko kimoja kisha koroga tena hadi mchangayiko wako uwe kama kinywaji.

Kunywa mchangayiko huo asubuhi kabla hujala kitu chochote au unaweza kunywa mchangayiko huo kila baada ya mlo mkubwa au ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, mchanganyiko huo husaidia usagaji wa chakula na uondoaji wa sumu mwilini.

Katika kutekeleza mpango huu kwa lengo la kupunguza unene, usisahau kuzingatia suala la ulaji wa vyakula vyenye faida mwilini na vinavyoruhusiwa kiafya. Itakuwa ni kazi bure iwapo utatumia tiba ya asali huku ukiendelea na ulaji wa vyakula usiyokubalika kiafya. Halikadhalika mazoezi ya mara kwa mara ni suala muhimu kuzingatiwa.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx