Na.Sheila Samba & Abushehe Nondo,Maelezo
Viongozi
wa Dini nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala
kuwapuuza viongozi hao ambao wamemuomba kukutana naye, kama inavyoenezwa
na baadhi ya vyombo vya habari.
Akizungumza
leo jijini, Dar es Salaam na waandishi wa habari Sheikh wa Mkoa wa Dar
es Salaam Alhad Mussa Salum, amesema taarifa zilizochapishwa na gazeti
la Tanzania Daima la Septemba 21 ISSN 0856 9762 toleo na.4310 sio za
kweli.
“Taarifa
hizo sio za kweli, taarifa hizo zimelenga kumgombanisha Rais na
Viongozi wa Dini na watanzania kwa ujumla na hilo halitafanikiwa,”
alisema Sheikh Alhad
Aidha
Viongozi hao wamesema uamuzi wao wa kumuomba Rais kuonana naye,
haujatokana na kuagizwa na UKAWA, bali umetokana na maono waliyopewa na
Mwenyezi Mungu.
Amefafanua
kuwa Rais MAGUFULI anawaheshimu Viongozi wa dini na mara zote amekua
akiwaomba wamuombee na kusema leo ni siku ya tano tangu wamuandikie
barua ya kumuomba kukutana naye na wanaimani Rais atakutana na Viongozi
hao.
Ameeleza
kuwa Barua hiyo imeandikwa Septemba 19 na kupelekwa siku hiyo hiyo
Ikulu, ikiwa imesainiwa na Katibu Mkuu wa Bakwata, Katibu Mkuu wa CCT na
Katibu Mkuu wa TEC.
“Naomba
watanzania wasisikilize maneno hayo kwasababu hayana nia njema kwa
Taifa letu, naamini Mh Rais tutaonana nae na tutaongelea mustakbali wa
nchi katika mambo mbalimbali,” alisistisa Sheikh Alhad
Akizungumzia
utendaji wa Serikali ya Rais MAGUFULI, Sheikh ALHAD amesema Rais
amerejesha nidhamu Serikalini, ukusanyaji mapato umeimarika na pia pengo
kati ya wasionacho na walionacho linaanza kupungua.