Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akipokea msaada wa chakula kutoka kwa Mhe. Leontine Nzeyimana, Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya Burundi kwa ajili ya Waathirika wa tetemeko la ardhi huko Mkoani Kagera. Msaada huo ni pamoja na mchele tani 100, sukari tani 30, mahindi tani 50 na majani ya chai tani 3.
Mhe. Dkt. Kolimba akitoa shukrani za dhati kwa niaba ya Serikali kwenda Serikali ya Burundi baada ya kupokea msaada huo wa chakula.
Mhe. Dkt. Kolimba akiwa katika picha ya pamoja Mhe. Nzeyimana na wadau wengine. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu akifuatiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi.