Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli leo hii ametengua uteuzi wa Afisa Tawala Mkoa Kagera,RAS na DED Manispaa ya Bukoba kwa kufungua akaunti nyingine isiyorasmi yenye jina linalofanana na akaunti halali ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Pia katika hatua nyingine Rais Magufuli amepokea msaada wa TZS milioni 545 leo kutoka ubalozi wa India kwa lengo la kuwasaidia walioathirika na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.TAARIFA RASMI YA HABARI HIZI SOMA HAPO CHINI.