test

Jumatatu, 26 Septemba 2016

Mwnafunzi kidato cha tatu afa maji ziwani akijifunza mambo ya utalii


JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limesema kifo cha mwanafunzi wa kidato cha tatu, Yahaya Rashida (19) aliyekufa maji katika ziwa Nyasa mkoani humo kimesababishwa na uzembe wa walimu waliokuwa wameambatana naye, pamoja na wanafunzi wengine ili kujifunza mambo ya utalii katika ziwa hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Zubery Mwombeji, tukio hilo lilitokea Septemba 23, mwaka huu majira ya saa 11:00 jioni katika mji mdogo wa Mbamba bay wilayani Nyasa.
Alisema mwanafunzi huyo aliyepoteza maisha alikuwa akisoma katika shule ya sekondari Matika.
Ni mkazi wa Mbinga Mjini. Mwombeji alisema Rashid alikuwa ameambatana na wanafunzi wenzake pamoja na walimu wa shule hiyo waliokwenda wilayani Nyasa, kwa lengo la kujifunza masuala ya utalii, mawimbi ya ziwani pamoja na mipangilio ya miamba iliyopo katika ziwa hilo.
"Usimamizi wa walimu waliokuwa wameambatana na hawa watoto haukuwa mzuri ndio maana ulisababisha mtoto huyu kufa maji, kwa sababu baada ya kumaliza mafunzo yao ndipo walikuja kubaini nguo na viatu vikiwa mchangani ufukweni wakati mwanafunzi mwenyewe akiwa hayupo ", alisema.
Alisema baada ya kuona mwanafunzi huyo haonekani, walikwenda kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Nyasa na Polisi kwa kushirikiana na wavuvi walianza kazi ya kuutafuta mwili wa marehemu na kufanikiwa kuupata Septemba 24, mwaka huu, majira ya saa 5:00 asubuhi.
Hata hivyo, alisema mwili huo ulipatikana ukiwa chini ya maji na kufanikiwa kuutoa nje ya ziwa hilo na kuukabidhi kwa viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga kwa ajili ya kuendelea na taratibu za mazishi. Alisema uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx