Mwanamuziki
Fulgency Mapunda maarufu Mwanacotide na mtayarishaji wa muziki, Mussa
Sikabwe wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakidaiwa
kusambaza wimbo kwenye mtandao wa YouTube wenye maudhui ya kumdhalilisha
Rais John Magufuli.
Wakili
wa Serikali, Dereck Mukabatunzi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Thomas Simba kuwa Agosti, eneo la Manzese wilayani Kinondoni,
washtakiwa walisambaza wimbo huo wenye maudhui ya ‘Udikteta uchwara.’
Baada
ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa walikana na upande wa mashtaka
ulidai upelelezi haujakamilika. Kesi iliahirishwa hadi Oktoba 12,
itakapotajwa.