Kamati
ya Utendaji ya Taifa ya Chama cha Wananchi (CUF), imeandaa ajenda ya
kumfikisha Prof. Ibrahim Lipumba mbele ya baraza kuu la uongozi wa chama
hicho ili ajieleze kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja
na kuvamia ofisi.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Naibu
Katibu Mkuu wa chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui imesema kutokana na
kitendo cha kuvamia ofisi kuu ya chama hicho Jijini Dar es Salaam,
kusababisha uharibifu wa mali hivyo kesho kamati hii itakaa kwa ajili ya
kujua mustakabali wa chama hicho.
Mazrui
amesema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ya mwaka 1992 kamati ya
utendaji ya taifa imeandaa ajenda na kumfikisha Prof. Lipumba mbele ya
baraza hilo ili ajieleze kwa nini asichukuliwe hatu za kinidhamu kwa
mambo aliyoyafanya.
Katika
hatua nyingine Mazrui amesema kamati hiyo imekataa maoni na ushauri
uliotolewa na msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mtungi
ambaye amesema kuwa ofisi hiyo inamtambua Prof. Lipumba kama mwenyekiti
halali wa chama hicho.