test

Jumatano, 28 Septemba 2016

Kweli Lipumba ni Prof. Asema chombo chenye mamlaka ya kumvua uanachama ni Mkutano Mkuu wa Chama


Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu uamuzi uliochukuliwa na Baraza Kuu dhidi yake, Prof. Lipumba alisema chombo chenye mamlaka ya kumvua uanachama kiongozi huyo ni Mkutano Mkuu na si Baraza Kuu hata kama limeongozwa na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.


Alisema kabla ya kufikia uamuzi huo, Katibu Mkuu alipaswa kuitisha Mkutano Mkuu ambao pamoja na mambo mengine, ulitakiwa kumjadili ili wajumbe waweze kumpigia kura ya kumwondoa.

Prof. Lipumba, alisema baada ya kufanyika kwa kikao hicho, wajumbe wanapaswa kumjadili na kumpa nafasi ya kujitetea ili atakapomaliza waweze kuamua kama wanamfukuza ama laa.

“Kwa mujibu wa katiba ya CUF,  Baraza Kuu la Uongozi halina mamlaka ya kunivua uanachama mimi, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Bara, kutokana na Katiba yetu inavyojieleza. Chombo chenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Mkutano Mkuu na si vinginevyo,” alisema Prof.  Lipumba.

Alisema chama hicho kinaendeshwa kwa kufuata kanuni na katiba,  na si uamuzi wa watu wachache kwa masilahi yao binafsi, hivyo basi uamuzi wa kumfukuza uanachama haukuzingatia katiba ambao alisisitiza kuwa ni batili.

“Hakuna mtu au kiongozi anayeongoza chama kwa kufuata utaratibu wake binafsi, bali tunafuata kanuni na katiba ya chama ambayo ndio inayotoa mwongozo wa nini kifanyike ndani ya chama hicho,”  alisema.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx