Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania limesema liko tayari muda wowote na wakati wowote kukabiliana na majanga ya aina mbalimbali ya kivita yatakayotokea nchini kama vile ugaidi kutokana uimara madhubuti uliojengeka kwa jeshi hilo.
Hayo yamesemwa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania Luteni Venance Mabeyo wakati wa Ufunguzi wa zoezi la kivita kwa ajili ya maadalizi ya kuhitimisha kusherehekea maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ tangu kuanzishwa kwake siku ya tarehe 01 septemba mwaka 1964 maadhimisho yanayotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 30 mwezi huu huko Bagamoyo Mkoani Pwani huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli akitarajiwa kuwa mgeni Rasmi.
Akifungua mazoezi hayo ya kivita ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania Kamandi ya Wanamaji NAVY Luteni Venance Mabeyo amesema kuwa Jeshi la Tanzania ambalo linashikilia nafasi za juu kwa Ubora na umahiri wa kivita Duniani limeimarisha ulinzi wa kutosha katika mipaka yote ya nchi ikiwa ni njia ya kujihami kukabiliana na changamoto mbalimbali za kivita ikiwemo ugaidi ambao umekuwa tishio kwa nchi nyingi duniani pia katika kudhibiti Uharamia baharini.
Adha Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Wananchi Tanzania Davis Mwamunyange Luteni Mabeyo amewataka wanajeshi kujiweka tayari kwa vita kila wakati ikiwa pamoja na kujijengea `ujasiri,Ushupavu na umahiri wa kutumia zana za vita pamoja na kukumbuka wajibu wao wa kulinda mipaka ya nchi muda wote ili isiingiliwe na adui.
Katika zoezi hilo la mafunzo ya kivita kwa jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kamandi ya Wanamaji jumla ya ndege vita tatu zitashiriki pamoja na meli 8 zenye Teknolojia za kisasa za kivita.zoezi hilo licha ya kuwa maalum kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania pia sehemu ya mafunzo ya kujiweka tayari katika kukabiliana na adui sambamba na kupima uwezo wa zana za vita za jeshi hilo.