test

Jumapili, 18 Septemba 2016

CHIPS MAYAI NI HATARI SANA,WANANCHI WAONYWA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameonya juu ya madhara ya chips mayai Kupitia mtandao wa intaneti kuhusu chakula hicho maarufu nchini unaweza kukutana na maswali mengi.
Miongoni mwa maswali hayo ni; nani aliyekuja na ubunifu wa chips mayai? Kwa nini chakula hicho kimekuwa maarufu sana? Pamoja na kutoa ajira nyingi kwa vijana ni fursa gani zaidi zimetengenezwa na chips mayai kwa jamii? Nini faida ya chips mayai mwilini? Nini madhara ya chips mayai? Kwa nini watu hupenda zaidi zege lililotayarishwa na Wapemba?

Kwa nini wapika chips wengi ni wanaume? Na kwa nini zege likipikwa na mwanamke linadoda? Waziri Ummy amewataka Watanzania waache kula chipsi mayai kila siku kwa kuwa ni hatari kwa kiafya. Mabachela na wanafunzi vyuoni mpo?
Ametoa angalizo hilo mjini Dodoma wakati wa kufunga mafunzo ya wasimamizi na wadadisi wa utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi Tanzania wa mwaka 2016.
Amesema wananchi wale mlo bora wenye tija katika miili na si chipsi mayai a.k.a zege. Kuna wenye mtazamo tofauti na wa Waziri Ummy kwa maelezo kwamba, wanaotaja madhara ya ‘viepe yai’ waeleze pia faida ya chakula hicho pendwa.
Kudharau hatari ya chips mayai hakubadili ukweli kuwa, chakula hicho kina mafuta mengi na inadaiwa kuwa ni miongoini mwa vyakula vinavyopikwa kwa zaidi ya nyuzi joto 300.
Unapokula chips mayai tambua kuwa unaongeza kiasi kikubwa cha mafuta ambayo ni hatari kwa mwili wako na kama hufanyi mazoezi unakaribisha matatizo ya moyo hasa yanayotokana na kuziba kwa mirija.
Inadaiwa kwamba, mwili wa binadamu hautupi kinachofaa, kama hakitumiki huhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye na ndiyo maana unapokula vyakula vyenye mafuta mengi unaongezeka unene na uzito.
Unene ni chanzo cha magonjwa mengi kwa sababu ya wingi wa mafuta mwilini unaosababisha kuziba kwa njia za kusafirisha damu. Hali hiyo inasababisha nguvu ya ziada itumike kusukuma damu hiyo ili isambae mwilini hivyo kuongeza mapigo ya moyo. Mapigo ya moyo yanapoongezeka yana madhara na pia yanapopungua sana ni hatari.
Ingawa wengi wanapenda kula chips kwa sababu mbalimbali ukiwemo urahisi wa kuzipata, bei na mtazamo kwamba hazikinaishi, si busara kudharau tahadhari inayotolewa zikiwemo taarifa zinazodai kuwa, chakula hicho ni chanzo vifo vya ghafla, kinachangia kupunguza nguvu za kiume na kinaongeza kasi ya mwanadamu kuzeeka. Wapenda chips wanapaswa kubadilika, wasithamini utamu kuliko usalama wa afya zao.
Huhitaji elimu ya udaktari kufahamu kwamba, matunda na mboga mboga ni muhimu mwilini na si lazima uwe na Shahada kutambua kwamba, miongoni mwa maadui wakubwa kwa afya zetu ni sisi wenyewe. Siku njema.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx