test

Jumatano, 3 Agosti 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 7 & 8 ( Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


MTUNZI:EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA....

Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio na kujikuta nikianza kuomba sala ya kuniepusha na kukamatwa kwetu kwani ni muda mchache ulio pita baba alitoka kunionya kwa ujinga kama huo.Nikamtazama Salome na taratibu nikamuona mwenzangu akilegea kabla hajaanguka nikamuwahi kumkumbatia ili asianguke chini na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa.......

ENDELEA....

.....Nikaendelea kumshikilia Salome ambaye anahema Kwa pumzi za taratibu kutokana na giza sikujua kama ameyafumba macho yake.Mlango ukatingishwa kidogo kama mtu anayetaka kufungua na kuingia.

“Eddy…..Eddy”

Nikasikia ni sauti ya chini ya John ikiniita nje ya mlango, Nikawa na wasiwasi huenda atakuwa yupo na walinzi au mwalimu ili iwe rahisi kwa kunikamata endapo nitaitiaka.Akarudia kuniita tena ila nikakausha kimya nikamsikia akiendelea kufungua fungua vyoo vingine na baada ya muda sikumsikia tena.


“Salome Salo”

Nilimuita Salome huku nikimtingisha taratibu ila mwenzangu hakunijibu kitu chochote.Nikakumbuka baba alinipa simu nikaitoa mfukoni na kuiwasha nikammulika Salome nikakuta mwenzangu macho yake yamebadilika na kiini cheusi cha katikati ya jicho sikukiona na kulifanya jicho lake lote kuwa jeupe.Mwili mzima ukaanza kunitetemeka huku taratibu nikahisi umotomoto kwenye mapaja yangu na kuifanya suruali yangu kulowana nikajua moja kwa moja mtu mzima nimeshalimwaga mbele ya Salome ambaye sielewi amepatwa na nini.

Kwa jinsi miguu inavyotetemeka nikashindwa kuizuia hali ya kulimwaga kojo ambalo linachuruzika kwenye mapaja kwa kasi huku likiwa la motomoto na mbaya zaidi nimetoka kuchimba mgodi muda si mrefu na sikufikia mwisho wa uchimbaji.Kwa uzito wa Salome na kukosa kwangu muhimili wa kusimama nikajikuta nikianza kushuka chini taratibu huku mgongo ukiwa unaburuzika ukutani hadi nikakaa chini.   
Nikaendelea kumnong’oneza Salome ila mwenzangu hakuitika sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kumkumbatia huku kichwa chake akiwa amekilaza juu ya kifua changu,cha kumshukuru Mungu ni vyoo tulivyopo hakuna hata kimoja ambacho kimetumika kwani ndio kwanza vipya vinamsubiria diwani aje kuvizindua siku mili mbeleni.
Nikaanza kumlaani John kwa masihara yake nikahisi kwamba alikuja kunitania na utani wake umweniachia majanga ambayo sijui niyamalize vipi kwani hata kusimama ninashindwa kwa jinsi suruali yangu ilivyolowana na mbaya zaidi mwili mzima unanitetemeka

Nikatazama saa ya kwenye simu nikakuta ni saa tano kasoro usiku,nikaendelea kusubiri huku mara kwa mara nikiwa ninamtingisha Salome ili azinduke.Baada ya masaa mawili kupita huku nikiwa nipo macho gafla Salome akapiga chafya nikaiwasha simu na kummulika Salome usoni nikakuta anaanza kufumbua fumbua macho na matumaini ya kutokulala chooni yakaanza kunijia kwani nilishakata tama nikajua ni lazima nitalala chooni.

“Salome”
“Mmmm”
“Unajisikiaje”
“Mmmmm”
“Unajisikiaje….?”
“Kidogo afadhali”
“Unaweza kusimama?”
“Mwili hauna nguvu”

Ikanilazimu kusubiri ili Salome nguvu ziweze kumrudia.Masaa yakazidi kukatika huku kila nikimuuliza Salome juu ya kurejewa na nguvu anadai bado.Nikaanza kupata wasiwasi kwani hadi sasa hivi imesha timu saa tisa usiku.Kijimwanga kikaanza kuchomoza na kuingia katika uwazi wa chini katika choo.Nikashangaa Salome akikurupuka na kusimama kama mtu aliyekuwa akiota ndoto mbaya

“Eddy tupo wapi?’
“Chooni”
“Tupo chooni Eddy…..bwenini kwetu hawajachukuliwa rollcal?”Swali la Salome sikujua nilijibu vipi kwani hata mimi mwenyewe sikujua kama bwenini kwetu watu wamehesabiwa namba

“Salome cha msingi wewe uende mbwenini kwenu sasa hivi mambo mengine tutazungumza baadaye tukionana”
“Kwani ni saa ngapi Eddy?”
“Saa kumi na mbili kasoro”

Nikafungua mlango wa chooni nikachungulia nje,nikaona kupo salama hakuna mtu nikampiga busu Salome kisha nikatoka na kuelekee kwangu bwenini kwa ajili ya kujiandaa kwa ajili ya msomo.Nikamkuta John akiwa bado amelala sikutaka kumsumbua nikapanda kwenye kitanda changu ambacho kipo juu nikajilaza ili kuupuumzisha mwili ila nikakumbuka kuwa nimejikojolea.Nikaivua suruali pamoja na boxer yangu japo kuna baridi kali ila ikanilazimu kwenda bafuni kuoga

Nikarudi na kukuta watu wengine wakianza kuva nguo za darasani huku wengine wakiwa wanaelekea kupiga mswaki

“John vipi hebu amka kwanza?”
“Eddy mwanangu nina umwa?”
“Una umwa na nini?”
“Eddy wee acha tu mwanangu jana yaliyo nikuta nimakubwa”
Kwa jinsi ninavyo mjua John kweli nikagundua anauwmwa kwani hata kuzungumza kwake ni kwa shida

“Sasa nikufanyie mpango kwa Patroni(Mlezi wa kiume) akupeleke hospitali”
“Ndio mwanangu hapa sijielewi kabisa”

Nikavaa nguo za darasani na kwenda katika chumba cha Patron na kumueleza juu ya kuumwa kwa John.Ila Patron akaniomba nimsindikize John hospitali kwani yeye anakwenda kushuhulikia kumtafuta msichana mmoja aliye potea jana usiku.Moyo ukaanza kunienda mbio huku nikiwa na wasi wasi
“Patroni huyo msichana aliye potea ni wakidato cha ngapi?”
“Kidato cha tano”

Sikutaka kujitia mawazo kwani moja kwa moja msichana aliyelala nje ya bweni alikuwa ni Salome na kwa jinsi wasichana wanavyolindwa huwa huesabiwa kila mara wakati wa usiku nikamuaga Patroni na kutoka kwenda bwenini kumchukua John.
Nikaikuta hali yake ikiwa imezidi kuwa mbaya kwani mwili mzima ulikuwa ukimtoka jasho.Nikasaidiana na rafiki zangu wengine kumuwahisha John hospitali huku moyo ukianza kupata mashaka juu ya hali ya John.Tukafika hospitali ya shule akapokelewa na manesi na kumtundikia dripu la maji.

Wezangu wengine wakaenda darasani mimi nikabaki hospitali huku nikiwa na kazi ya kumfuta John jasho linalo mwagika huku wasiwasi ukizidi kunijaa juu ya afya ya John

“Eddy”
“Niambei ndugu yangu”
“Eddy ninakufa kaka”
“John hufi kamanda wangu”

John akacheka taratibu huku akinishika mkono huka anatetemeka.Nikazidi kupata wasi wasi huku machozi kwa mbali yakianza kunilenga lenga.Dokta akaanza kumfanyia John vipimo vyote ila hakumkuta na ugojwa wowote

“Eddy jana mwenzako ni….nili…..kuwa nipo na Clau…..”
“Ndio kaka”
“Tulikuwa darasa la kule chini basi kuna ki…..tu ki….linipiga kifuani il…a siku..jua ni ni..ni”
“Ikawaje kaka?”
“Nikaja kukufwata kule ulipo ila sikukupata wakati naru…I pale darajani nikao…….oo….oo..”

Gafla John akaanza kutingishika kama mtu mwenye kifafa huku akiwa amening’ang’ania mkono wangu.Manesi wakaanza kumshika ili kuutuliza mwili wake huku nikisaidiana naye.Machozi yakaanza kunimwagika kwani hali ya John ikazidi kuwa mbaya,Puvu jingi likaanza kumtoka huku puani akiwa anatokwa na damu
“ED…….”

John akajitahidi kuniita ila kinywa chake hakikuweza kufunguka na suati yake ikakata gafla na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa.Sikuweza kuyazuia machozi yangu baada ya kumuona John akiwa ametulia kimya kitandani huku vidole vyake vikiwa vinajifungua taratibu kwenye mkono wangu alioushika.

“John…..John…..John kaka please wake up you can not die brother you my soujor please”(John…..John……John kaka amka huwezi kufa kaka wewe ni mwanajeshi wangu tafadhali)

Nilizungumza huku machozi yakinitoaka nikiwa najitahidi kumtingisha huku kichwa chake kikiwa nimekiweka kwenye mapaja yangu.Dokta akampima John mapigo ya moyo na nikamuona akitingisha kichwa akimaanisha John amefariki dunia.
“John amka rafiki yangu nitasoma na nani mimi”

Manesi wanishika na kunitoa nje huku nikiona wakimfunika John kwa shuka mwili wake mzima.Nikazidi kuchanganyikiwa na kujua hiyo ndio safarai yangu ya mwisho ya kumuona rafiki yangu John ambaye kwangu amekuwa zaidi ya ndugu.Manesi wakanikalisha kwenye benchi huku wakiendelea kunibembeleza

Nikaona kundi kubwa la wanafunzi wa kike wa kidato cha tano likija hospitali huku wakiwa wamembeba mwenzao ambaye anaonekana kupoteza fahamu.Nikasimama na kumuona ni Salome aliye bebwa huku akionekana kuwa na hali mbaya kupita maelezo.......

                            ******SORY MADAM******(8

....Nikazidi kuchanganyikiwa sikujua Salome kimempata nini,Nikataka kwenda kumuuliza mmoja wa rafiki zake ila Nesi akanizuia kwa kunishika mkono.Nesi mmoja akaondoka kwenda kusaidiana na wanafunzi wa kike wa kidato cha tano na kumuingiza katika chumba cha wagojwa mahututi.Kila nilipojaribu kuyazuia machozi yangu nikajikuta nikishindwa na nikaendelea kulia hadi wanafunzi wa waliobaki nje wakanifuata kwenye benchi huku kili mmoja akiwa anahamu ya kutaka kujua ni kitu gani kinachoniliza

Nesi akanizuia nisizungumze chochote huku akiwa amenifunga mdomo kwa kiganja chake
“Jamani mwenzenu anaumwa nawaomba mkakae kule”

Nesi alizungumza na kuwafanya mwanafunzi mmoja baada ya mwengine kuondoka katika eneo nililopo kasoro Claudia ambaye anaonekana kuwa na mashaka

“Nesi Maria dokta anakuhitaji haraka”
Nesi aliyeniziba mdomo akanyanyuka haraka na kumfwata nesi mwenzake aliyekuja kumuita nikawaona wakiingia katika chumba alichoingizwa Salome.Claudia akaja kwa haraka hadi sehemu niliyokaa mimi huku naye machozi yakimwagika na akazidi kunichanganya akili kwani sikujua kinachomliza ni kitu gani.

“Eddy Salome anaumwa sana tena asana”
“Ooooh Mungu wangu naye anaumwa na nini?”
“Yaani hata sisi hatujui amekutwa ameanguka nje ya vyoo vipya kule chini huku damu zikimtoka puani”

“Ahaaa Mungu wangu ni nini hichi umefanya John naye amekufa,Salome naye aahaaa……Nakuomba Mungu usiwachkue wote”
“Eddy what are you say…..!?”(Eddy unasemaje……!?)
“John is dead”(John amekufa)

Nilizungumza kwa uchungu huku machozi yakinimwagika yakiandamana na makamasi yakinishuruzika katika pua zangu.Claudia akaachia ukulele mkali a kulia  huku akipiga hatua za kwenda walipo wezake huku akiwa anakimbia.Kwa bahati mbaya nikamshuhudia Claudia akikanyaga kamba ya kiatu chake cha shule na kumfanya miguu yake kugongana na kwa kasi kubwa akaanguka chini huku kichwa chake kikipiga kwenye ukingo wa msingi wa baraza ya kuelekea katika chumba alicho ingizwa Salome na kusababisha damu nyingi kuanza kusambakaa chini kwenye mchanga.

Nikanyanyuka kwa haraka na kwenda kumuangalia Claudia na kukuta akiwa yupo katika kauli ya mwisho huku akiwa ananiomba msaada nimnyanyue.Kila mwanfunzi aliyekuja katika eneo hilo nikamuoana akiondoka huku akilia na wengine wakiwa wanaziba macho yao wasione kilichotokea kwani ubongo uliochanganyikana na damu ulitapakaa chini huku mimi nikawa kama nimepigwa butwaa.

Madaktari wawili wakaja tulipo simama huku wakishangaa ni kitu gani kimetokea,Mmoja akaniuliza swali ni kipi kilicho mpata Claudia sikuwa na chakumjibu kwani mdomo wangu haukuweza kufunguka.Nikaanza kupata wasi wasi na kwa mwendo wa haraka nikaenda katika chumba cha wagojwa mahututi nikaufungua mlango kwa nguvu na kumstua nesi anayemalizia kumfunika Salome shuka kichwani kwa shuka la kijani….Nesi akajaribu kunizuia huku akiniomba nitoke nje nikajikuta ninamsukuma na kwenda kwenye kitanda alicho lazwa Salome na kumkuta mwili wake umekuwa wa baridi huku macho yake yakiwa yamejifumba.Nikamtingisha huku nikimuita

“Salome mpenzi na wewe unakufa ni nani atabaki na mimi eheee amka mpenzi tafadhali”

Salome hakunijibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya kama nilivyomkuta nikarudia kumtingisha ila sikupata jibu.Nikaanza kulia huku nikilitaja jina la Salome

“Salome Salome nakupenda mpenzi wangu yaani penzi letu limedumu kwa masaa please baby amka basi hata nione kicheko chako”

Maneno yangu hayakuwa na nguvu ya kumrudisha Salome duniani,nikashtukia kitu chenye ncha kali kikinichoma mgongoni,nikageuka taratibu na kukuta nesi akichomoa bomba lenye sindano na taratibu macho yakajawa na usingizi na kichwa changu nikakiangushia kwenye kifua cha Salome


                                               *****

“Wewe fala Eddy”

Nikastuka huku nikinyanyuka kwa hasira nikitaka nimpige mtu aliye nitukana na kumkuta ni John,Moyo wangu ukanipasuka na kunifanya nianze kurudi nyuma huku nikiwa nina muogopa

“Eddy jana umepiga bao ngapi best hadi umeshindwa kurudi bwenini?”

John aliendelea kunisemesha na kunifanya nizidi kuchanyanyikiwa na kuanza kujiuliza kama nipo peponi mbona John mwenzangu amevaa nguo za shule na sote tupo bwenini isitoshe kama kawaida yake anatukana kiasi kwamba amenikasirisha

“Eddy mwangu saa hizi saa moja kamili wewe bado umelala tena unaota unatupigia kelele za kumtaja Salome wako hapa…….Kumbe Eddy na ujanja wako wote unaweza ukamuota demu?”

Jonh akaanza kucheka huku akinitazama nikayazungusha macho yangu chumba kizima nikamuona John peke yake,Nikajitazama nguo nizizo zivaa nikastuka kuona ni nguo za jana nilizozivaa prepo na sehemu niliyo kaa ni juu ya kitanda changu

“John nipo wapi?”
“Eheee wewe Eddy leo hii unaniuliza upo wapi kwani rafiki yangu wewe unavyohisi au unavyoona upo wapi wewe?”
“Nina maana yangu kukuuliza nipo wapi?”

“Best upo kwenye Air Force One ya Obama”
 John alizungumza huku akizidi kucheka hadi akakaa kwenye kiti kilichopo ndani ya chumba chetu
“Aisee Mazee bado mnajichekeshachekesha hapa tokeni nataka kufunga milango”

Patron alizungumza huku akiwa ameshika funguo nyingi kwenye mkono wake wa kushoto
“Patroni tunaomba dakika kumi jamaa avae nguo”
“Nakwenda mabweni ya O level nikirudi nisiwakute”
“Sawa Patron…….Oya Eddy hebu amsha ke**e zako hapo juu tumeshachelewa assemble”

Nikashuka kitandani na kusimama chini na kusogelea John na kumgusa mkono nikaona ni John kweli kwani hana mabadiliko yoyote ikanibidi kutoka nje kuangalia mandhari nikayakuta ni bwenini na mbaya zaidi nikamuona mwalimu wa zamu akiwafukuza wanafunzi wa vidato vyengine ili wawahi mstarini huku akiwa anawachapa

“Oya John mfumuko huyo anakuja”
“Yuko wapi?”
“Bweni la form four kule”
“Oya mwanangu hembu vua basi hizo nguo zako fasta tuondoke na jamaa lilivyo na mijisifa lile litatucharaza bakora humu humu”

Ikanibidi nikubaliane na hali halisi kuwa John hakufa nikaanza kuivua surualia yangu haraka haraka huku John akifugua begi langu la nguo na kunitolea nguo za shule

“Alafu Eddy mwanagu umelimwaga eheee?”
“Kwanini?”
“Wewe huoni suruali yako ilivyo chora mchoro hapo mbele sijui ni ramani ya kuendea wapi”
“Mwanangu wee acha tu yaliyonikuta jana mmmmmm……”
“Alafu jana ninakuja kukustua kwenye vyoo kule mwangu upo na huyo demu wako ukanikaushia”
“Unajua wewe ndio chanzo cha kunifanya nirudi hapa saa kumi na mbili”
“Weee umerudi saa kumi na mbili?”
“Ndio jana dogo alizimia”

Mwalimu Mfumuko akaingia chumbani kwetu huku mkononi akiwa na fimbo ya muanzi

“Munafanya nini?”
“Ticha jamaa anamalizia kuvaa mara moja”
“Munajua nyinyi Adivance muna jeuri sana.Munataka kuifanya hii shule kama wamejega baba zenu si ndio…….Nyoosha mkono”

Mwalim mfumuko akaishika fimbo yake vizuri na kumchapa John fimbo mbili za mkononi.Kisha na mimi akanichapa fimbo mbili za mkononi
“Sasa ole wenu niende nirudi niwakute hapa”

Akatoka na kutuacha ndani,Nikabadilisha boxer nikvaa nyingine safi,Nikajipilizia BODY SPRAY mwili mzima kisha nikavaa nguo zangu na kujiweka sawa.Nikachukua begi langu la madaftari na safari ya kuelekea shule ikaanza kwani mabweni yetu yapo mita chache kutoka shule ilipo.Tukaingia kwenye darasa moja kwa ajili ya kujificha kwani wachelewaji wote wa mstarini wanachapwa na mwalimu aliyesimama katika eneo ambalo huona kila mwanafunzi anayeingia katika eneo la mastarini

“Eddy na mwenzako mnafanya nini huku wakati wenzenu wapo Assemble?”Madam Rukia alizungumza huku akiiingia kwenye darasa tulilo jificha na kutufanya tukae kimya
“Alafu Eddy wewe mtoto mbona unamatatizo hivyo yaani hufananii na ukorofi unaoufanya?”
“Madam you know……”(Madam Unajua……)

“Najua nini wakati wewe umejificha na huyu mwenzako huku.Hebu waangalie macho yenu yanavyowawaka kama ya bundi”
“Rukia wana tatizo gani hao?”
“Sir Masolwa hawa vijana nimewakuta wamejificha huku wakati wezao wapo mstarini”
“Njooni…..Tena huyo mrefu si ndio alimgomea mwalimu Kikole?”
“Ndio yeye mwalimu yaani huyu kijana sijui ana matatizo gani”

Mwalimu Masolwa akatuamuru tulale chini kisha kila mmoja akatuchapa fimbo nne nne za nguvu.
“Nahitaji mkafyeke nyasi zote zinazoelekea barabara ya getini.Mtafuteni kiranja wa Stoo akawape makwanja na ole wenu mkimbie hiyo kazi mtanijua mimi ni nani.Poteeni mbele ya macho yangu”

Tukaondoka na kwenda mstarini na kukuta watu ndio wanaondoka kuelekea kwenye madarasa yao.Salome alipo niona akanifwata na tukasimama pembeni

“John yule kiranja yule pale muwahi basi atufanyie mpango wa makwanja”
“Eddy mambo mpenzi wangu?”
“Safi vipi kwema?”
“Kwema tu ulifika salama bwenini?”
“Ndio vipi wewe jana hamjahesabiwa?”
“Jana hatujahesabiwa nahisi Matroni aliogopa giza.Alafu mwezio bado nina hamu kama nini?”
“Usijali zitakwisha hapa tumepewa adhabu ya kwenda kufyeka”
“Mmefanyaje?”
“Tumechelawa kuja hapa”
“Yaani Eddy mpenzi wangu natamani hapa nikirukie tufanye hata hapa”
“Hebu acha utoto..Claudia yupo wapi?”
“Anamalizia kudeki kibaraza cha bwenini kwetu”
“Ahaa powa bwana ngoja sisi tukafyeke tutaonana baadaye”
“Powa! I love you”
“Love you too Salome”

Tukaachana kila mmoja akaelekea sehemu yake huku akili yangu ikianza kuifikiria ile ndoto mbaya niliyoiota,Kila nikimuangalia John ninajihisi kulia lia huku hali hiyo ikiwa sawa ninapomuangalia Salome.Tukaelekea sehemu aliyotuagiza  mwalimu Masolwa kufyeka,Tukaanza kufyeka huku tukiwa tunapiga story

“Eddy yule Salome ni mtamu?”
“Tena sana nanilio yake inajoto kama nini?”
“Weee mjinga kweli kwani hizo naniliu za wengine hazina joto?”

“Joto lina tofautiana wewe kuna wengine joto lake si kali kivile na huwa hazina utamu kivilee ila za wenye joto hata kama hujui ku Duu lazima tuu kiuno kitacheza”
“Nyoo yako ni hayo tu”
“Vipi na wewe Claudia?”

“Ahhaa jana kazingua yule.Pale umeme ulivyo katika nikamfwata kule madarasani kwao.Nikashindwa kumuomba hata mchezo nikajikuta ninamuomba tochi ndio niliyokuja nayo kule mlipo”

Nikaanza kumcheka John kwa sauti ya juu na kumfanya Mr Kikole anayepita katika barabara inayotoka getini kuelekea shule kunitazama.Kicheko kikazidi kuongezeka nilipo muona Mr Kikole na nikajikuta nikilikumbuka tukio lake la kujikojolea jana ofisini.Akanitazama kwa macho ya unyonge kisha akaendelea na safari yake ya kuelekea shuleni

“Mbona unacheka sana wewe kuomba tochi ndio unacheka kiasi hicho?”
“John sikucheki wewe”
“Ila?”
“Unajua jana si nilikuambia kuna story nitakuambia iliyonikuta ofisini?”
“Ndio”
Nikaanza kumuadisia John kila kilichomkuta Mr Kikole hata kabla sijamaliza John akakaa chini huku akicheka huku akipiga piga ngumi chini
“Eddy utanivnja mbavu zangu”

“Kweli John jana mtu mzima alilimwaga…..Tena alilimwaga pale bro alipojidai anapiga simu kambini akiomba msaada wa defender ili amchukue Best kumbe hata yule Kikole ni muoga”

"Chezea mjeda nahisi kwenye akili yake alikuwa akifikiria jinsi ya kwenda kuruka kichura chura na pombe anazo kunywa angekufa”
“Alafu nasikia hanywi bia anakunywa mataputapu?”
“Mwenyewe ndio ninavyosikia”
Tukaendelea na kazi ya kufyeka huku tukipiga story mbali mbali ila nikajizuia kumuadisia John nilicho kiota.Hadi inafika mida ya saa nne bado hatukumaliza kufyeka eneo zima.Akapita Madam Rukia ikanibidi nimuite

“Madam wapi hiyo?”
“Ndio Kiswahili gani hicho?”
“Ok! unakwenda wapi?”
“Unataka kujua ili iweje?”
“Nilidhani unakwenda kwa Madam Mery ninataka kwenda kumuona”
“Ninakwenda kwanza kwangu kisha nitakwenda kwa Mery”
“Kwani ametoka hospitali?”
“Amenipigia simu hii asubuhi kuwa amesharuhusiwa”
“Madam tunaomba basi twende tukamuone mara moja”

Madam Rukia akajifikiria kwa muda kisha akakubali,tukayaficha makwanja yetu  kwenye michongoma kisha tukaongozana na Madam Rukia.Tukapita getini pasipo kuulizwa na walinzi kwani tumeongozana na mwalimu ambaye yupo kwenye zamu

“Tena nimekumbuka twendeni kwangu mukanisaidie kubeba trey za mayai ili tuzipeleke kwa Mery”
“Sawa”

Tukaelekea nyumbani kwa Madam Rukia na akatukaribisha ndani kwake mabapo ni pazuri.John kitu cha kwanza alichokiwahi ni kuchukua PAD za gemu  ya PLAY STATION ambayo mara nyinyi huchezwa kwa kupitia TV.Akawasha na kukuta ina CD ya Game ya mpira
“Oya Eddy njoo nikufunge funge”
“Utaweza”

Nikakaa karibu yake na kuchukua PAD nyingine na tukaanza kuchagua timu za kuchezesha huku Madam Rukia akiwa chumbani kwake hatukujua anafanya kitu gani.Akatoka akiwa amejifunga tenge huku sketi yake ikiwa imechomoza kwa chini kwenye tenge lake

“Haya nahitaji mmoja wenu aje anisaidie kuokota mayai kwenye mabanda ya kuku”
“Eddy nenda mimi hapa nilipo ninajihisi vibayavibaya”

Sikutaka kubishana na John taratibu nikanyanyuka na kuongozana na Madam Rukia hadi kwenye mabandaya ya kuku wake wa kizungu(Kuku wa mayai).Uzuri wa nyumba anayoishi Madam Rukia imezungushiwa ukuta mrefu ambao si rahisi kwa vibaka kuingia na kuiba kuku.Tukaanza kuokota mayai huku tukiyaweka kwenye kindoo kidogo

“Eddy nasikia wewe ni mtaalamu”
“Mtaalamu wa nini?”
“Ahhhaa unajua ila unataka kuwapa kuku faida”
“Sasa Madam kama ningekuwa ninajua si ningesema”
“Hebu tutoke kwanza kwenye hawa kuku twende tukachukue trey za mayai”

Tukatoka nje ya banda la kuku na kuingia kwenye chumba kimoja kisicho na kitu kingine zaidi ya trey za mayai zipatazo hamsini

“Madam hapa unaishi na nani?”
“Peke yangu sema hii nyumba bado mpya ila siku si nyingi itahamia watu”
“Ni yako?”
“Hapana ni ya mzee mmoja hivi wa kichaga”
“Sawa”

Madam Rukia akanitazama kwa sekunde kadhaa huku akiwa kama anahitaji kuzungumza kitu ila akawa anashindwa.Akalifungua tenge lake na kubaki na sidiria huku akiniomba nimkune mgongoni.Nikaanza kumkuna mgongoni taratibu kwa kucha zangu ndogo ndogo.Akaniambia nishushe mkono hadi chini chini kwenye kiuno nimkune sehemu hiyo.Nikafanya huku nikimeza vijimate vya uchu,Taratibu nikaushusha mkono na kuuingiza kwenye sketi yake sehemu ya nyuma kwenye makalio yake.

Madam akageuka na kunishika shingo huku taratibu tukaanza kunyonyana denda,Nikamfungua sidiria yake na kuanza kuzitomasa chuchu zake taratibu taratibu.Nikaishika zipu ya sketi yake iliyopo nyuma na kuanza kuifungua kwa kwenda chini kisha sketi yake akaishusha haraka haraka huku nami nikivua shati langu la shule
“Oya mwanagu Eddy Tanesco wamekata umeme bwana”

Tuliisikia sauti ya John kwa nje na kunifanya nichungulie kwenye dirisha nikamuona John akiwa anaelekea kwenye mabanda ya kuku huku akichungulia chungulia ndani ya mabanda hayo akionekana kututafuta sisi.....
 ITAENDELEA....

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx