SERIKALI imepiga marufuku usafirishaji wa magogo nyakati za usiku sambamba na matumizi vya vyaraka vivuli kama sehemu ya kukabiliana na ukwepaji wa kodi inayotokana na mazao ya misitu nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amefikia hatua hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa mazao ya misitu kwenye mnada wa vitalu nane vya miti, shamba la Lunguza wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
Katika mnada huo ambao jumla ya shilingi bilion 2.2 zilipatikana Profesa Maghembe akazungumza na wafanyabiashara.
Kuhusu kusafirisha magogo nyakazi za usiku Profesa Maghembe amepiga marufuku sambamba na kutumia nyaraka vivuli kusafirishia bidhaa hivyo.
Jumla ya shilingi bilioni 2.2 zilipatikana kwenye mnada huo tofauti na matarajio ya serikali ya kukusanya shilingi bilion 1.3 kwenye vitalu nane vya shamba hilo la miti la Lunguza wilayani.