Muimbaji huyo ambaye alikiri wimbo huo kumwimbia aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Shilole, amekiambia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha EATV kuwa hakuwa na wazo la jina la wimbo huo mpaka AliKiba alivyozungumzia ‘Jike Shupa’ kwenye chorus na wimbo huo.
“AliKiba ndiyo kila kitu, yeye ndiye aliyetoa neno la ‘Jike Shupa’,” alisema Nuh. “Wimbo kanikuta nimeshaurekodi na nimeshafanya chorus yangu, na sikutaka kuiachia nikaenda kumshirikisha AliKiba akaniambia nyimbo imekamilika nitaingiza nini humu, na nyimbo nzuri nikamwambia no, kwa sababu nimekaa kimya muda mrefu nahitaji utofauti kwa sababu sijawai kufanya kolabo, basi akasema okey, tukaenda studio tukamute chorus yangu AliKiba akaingiza yake, ambapo katika kuandika kwake akaimba neno ‘Jike Shupa’, kwa hiyo tilte ya nyimbo Ali anahusika,”
Wimbo huo umefanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na kumtambulisha rasmi Nuh Mziwanda katika muziki wa bongofleva.