Mkazi
mmoja wa jijini hapa, Said Shomari (64) amehukumiwa kifungo cha miaka
15 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki silaha kinyume cha
sheria.
Shomari ambaye ni fundi saa, alitiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu hiyo na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo baada ya mshtakiwa kukiri kosa hilo. .....

Alikiri
kutenda kosa hilo jana alipopandishwa kizimbani mahakamani hapo na
Wakili wa Serikali Adolf Mkini kumsomea mashtaka yaliyokuwa yakimkabili
kwa lengo la kumkumbusha, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya
usikilizwaji.
Katika
kesi hiyo, Shomari alishtakiwa na mtoto wake, mfanyabiashara Ramadhani
Said (40), kwa makosa mawili, moja la kukutwa na silaha na la pili la
kukutwa na risasi bila kibali na kinyume cha sheria.
Katika mashtaka hayo, Shomari alikiri kosa moja la kumiliki silaha na akakana kosa la kumiliki risasi kinyume cha sheria.
Hata
hivyo, wakati Shomari akikiri kutenda kosa hilo moja na kuhukumiwa
adhabu hiyo, mtoto wake alikana kutenda makosa hayo yote.
Awali,
akiwasomea mashtaka hayo, Wakili Mkini alidai kuwa Novemba 9, 2015,
eneo la Kigogo, wilayani Ilala, mshtakiwa alikutwa akimiliki bastola
moja ndogo pamoja na risasi moja bila kuwa na kibali.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo na kuulizwa kama ni kweli au si kweli, ndipo alipokiri kutenda kosa hilo kwa kujibu kuwa ni kweli, hivyo Mahakama ikamtia hatiani.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo na kuulizwa kama ni kweli au si kweli, ndipo alipokiri kutenda kosa hilo kwa kujibu kuwa ni kweli, hivyo Mahakama ikamtia hatiani.
“Kwa
kuwa mshtakiwa amekiri kutenda kosa kwa shtaka linalomkabili, Mahakama
inamtia hatiani na kumhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela.”, alisema hakimu Mashauri.
Baada ya kutoa hukumu hiyo aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 15, mwaka huu, wakati kesi hiyo itakapoendelea kusikilizwa shtaka moja kwa upande wa Shomari na mashtaka yote mawili kwa upande wa Ramadhani.