Mwenyekiti
wa Bodi ya Parole ambaye pia ni Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema
amemtaka Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akubali kwamba alishindwa
katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na akae kimya hadi mwaka 2020.......
Mrema
aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam na kusisitiza kwamba alimtaka
Waziri Mkuu Mstaafu watoke CCM pamoja kwa kuwa nguvu ya upinzani ilikuwa
kubwa sana.
‘’Mimi
nitamuuliza 1995 wakati natoka nilikuambia tutoke sasa maji yamechemka
tukiweka unga tutakula ugali ukagoma, ukasema unaendelea kula kidogo
hadi alipojiuzulu akaendelea na CCM hadi alipotaka kugombea Urais
akakataliwa na wenzake ndipo akaja upinzani’’
Mrema
aliongeza kwamba Chama cha Mapinduzi kilitakiwa kuondoka madarakani
mwaka 1995 ambapo yeye ndiye alikuwa na nguvu kubwa ya kisiasa nchini.
Aidha
Mrema amewataka vijana kuwa makini na upinzania kwa kuwa Lowassa
alijiunga na upinzani baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea Urais ndani
ya CCM hivyo wajiepushe na maandamano kwani hayana faida kwao.