MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi wilayani Urambo mkoani Tabora, imemuhukumu Deus
Barnaba(45) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkuta na hatia ya
kumnajisi mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka tisa.
Akitoa
hukumu hiyo mwishoni wa wiki iliyopita, Hakimu Mkazi, Baptista
Kashusha, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande
wa mashitaka hivyo kumuona mshitakiwa ana hatia.
Alisema
adhabu hiyo iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kufanya vitendo
hivyo. Hakimu Kashusha alisema mashahidi nane walioletwa mahakamani hapo
walithibitisha kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo.
Mashahidi
hao ni pamoja na daktari aliyempokea mlalamikaji na kutoa fomu namba
tatu (PF3) iliyoonesha kuwa binti huyo aliumizwa katika sehemu za siri.
Awali,
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, ,Joseph Mbwana, alieleza mahakama hiyo
kuwa Machi 27, mwaka huu, majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha
Mwangaza wilayani Urambo, Deus alimnajisi binti mwenye umri wa miaka
tisa na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.
Aidha,
aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili kukomesha matendo
ya ubakaji kabisa kwani mtuhumuwa anaonekana ni mtu mwenye akili
timamu, alifanya hivyo kwa makusudi tu.
Hata
hivyo, mshitakiwa huyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwakuwa ni
mkosaji wa mara ya kwanza na ana wazazi, mke na watoto wanaomtegemea.