MVUA kubwa isiyo ya kawaida imeendelea kunyesha katika Jiji la Beijing China na kusababisha mafuriko ambayo yameuwa watu zaidi ya 200 na wengine mamia hawajulikani walipo huku nyumba zaidi ya 68,000 zikibomolewa na kusababisha zaidi ya watu milioni 16 kupoteza makazi yao.
Picha nyingi zilizopigwa zinonesha mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo Jumatatu Julai 25, imeathiri zaidi maeneo ya Jimbo la Shaanxi lililopo katika Mji wa Xi’an, Kaskazini mwa China.
Picha zinaonesha maji kujaa kwenye makazi ya watu huku mali zao zikiwa zinaelea yakiwemo magari na wengine wakibebana ili kuvuka kutoka eneo moja kwenda jingine.
Mvua hizo zilianza kunyesha tangu Jumatatu iliyopita na imesababisha maafa makubwa sambamba na kuahirishwa kwa mechi ya mahasimu wawili wa Jiji la Manchester Uingereza, Manchester United na Manchester City kutokana na uwanja kujaa maji. Mechi ilitarajiwa kuchezwa usiku wa kuamkia leo.