test

Ijumaa, 24 Juni 2016

Waziri mkuu wa uingereza David Cameron atangaza kujiuzulu


WAZIRI Mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya.
Akionekana mwenye majonzi mazito, Cameron amesema atajiuzulu katika siku 90 zijazo kutokana na matokeo hayo aliyoyaita kuwa ni ya kusikitisha. Cameron ambaye ameongoza kampeini ya kubaki ndani ya Umoja wa Ulaya (EU) amesema matokeo hayo yamemshtua pamoja na dunia kwa ujumla.

Akitangaza maamuzi hayo mbele ya waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Cameron amesema anajiona sio mtu muhimu tena wa kuiongoza nchi hiyo kutokana na uamuzi uliofanywa na raia wa taifa lake.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx