Kumekuwa
na mgogoro wa muda mrefu wa ardhi katika eneo la Mabwebande Dar es
salaam ambao unamhusisha Waziri mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na
wananchi.
Baaada ya
juhudi mbalimbali za kutafuta suluhu ya kudumu, uongozi wa Mkoa wa Dar
es salaam na Wilaya ya Kinondoni umemuomba Waziri wa ardhi, William
Lukuvi kufika kwa ajili kumaliza mgogoro na kuupatia suluhu ya kudumu.
Eneo la
shamba linalomilikiwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye linadaiwa
kuwa wananchi walilivamia baada ya kuona haliendelezwi kwa muda mrefu
na kuweka makazi katika shamba hilo lenye hekari 33. Akizungumza na Ayo
TV, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema…….
>>>’Mzee
Sumaye anamiliki shamba la hekari 33 ambalo halijaendelezwa tangu 1990,
jambo ambalo limefanya wananchi zaidi ya 1800 wakiangaika kutafuta
makazi katika eneo hilo la shamba‘
>>>‘Waziri
Lukuvi atafika katika eneo la Mwabepande kwa ajili ya kuleta ufumbuzi
wa kudumu wa mgogoro huu ambao tumekuwa tukiushughulikia kwa muda mrefu’
