JUKWAA la Wahariri Nchini (TEF), limewataka wanahabari kuwa makini na maisha yao wakati huu wa mchakato wa uchaguzi sambamba na kulaani kitendo cha vijana wa Chadema cha kumshambulia na kumpiga mwandishi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Christopher Lissa.
Aidha,
limewataka vyama vya siasa na watu binafsi wanaoandaa mikutano ya
waandishi wa habari kutowaalika makada wa vyama vyao ambao si
wanataaluma katika mikutano hiyo.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda alisema
kitendo cha kumpiga mwandishi wa habari hakivumiliki, kwani ni sawa na
kuipiga na kushambulia taaluma nzima ya wanahabari.
Alisema
tukio la kupigwa Lissa ni mwendelezo wa vitendo vyenye mwelekeo wa
kuwazuia waandishi wa habari kutekeleza wajibu wao wa msingi wa
kukusanya taarifa na kuuhabarisha umma wa Watanzania.
“Ifahamike
kuwa vitendo vya watu kuwashambulia waandishi wa habari wakiwa kazini
siyo tu vinakwaza utendaji wao wa kazi, bali vinadhalilisha utu wao
mbele wa jamii inayowazunguka."
Kibanda
alisema huu ni wakati wa waandishi wa habari kuchukua tahadhari wakati
wakiripoti matukio ambayo yanaweza kusababisha vurugu na madhara kwao na
kwa vitendea kazi kama kamera, magari.
“ Hakuna habari yenye thamani zaidi ya maisha yako mwandishi wa habari,” alisisitiza.
Kibanda amevitaka vyama vya siasa kama taasisi, viongozi, wanachama na wapenzi wa vyama hivyo, kuacha mara moja vitendo vya kuwashambulia waandishi wa habari kwa sababu zozote zile na kama vitendo hivyo vitaendelea hawatasita kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kususia matukio na mikutano yao.
Kibanda amevitaka vyama vya siasa kama taasisi, viongozi, wanachama na wapenzi wa vyama hivyo, kuacha mara moja vitendo vya kuwashambulia waandishi wa habari kwa sababu zozote zile na kama vitendo hivyo vitaendelea hawatasita kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kususia matukio na mikutano yao.
“
Tukiona vitendo hivi vinaendelea TEF kwa kushirikiana na taasisi
nyingine za kihabari haitasita kuchukua hatua zaidi dhidi ya vyama
husika na ikibidi, kususia matukio na mikutano ya vyama hivyo.
"Hatutaki
kuona waandishi wa habari wanakuwa punching box kwani urafiki wa
mwandishi wa habari na mwanasiasa au mchumi ni wa kitaaluma, hivyo
hatutamvumilia mtu awaye yeyote atakayeingilia msingi wa wanataaluma ya
habari ,” alisema.
Akihojiwa
juu ya taarifa hiyo ya TEF, kwa njia ya simu jana, Ofisa Habari wa
Chadema, Tumaini Makene alisema hawezi kujibu kwa simu kuhusu
walichokisema wahariri na kudai apewe muda wa kupitia taarifa hiyo ili
atoe jibu lenye uhakika.
Mwishoni
mwa wiki, Mwandishi wa UPL, Lissa alipigwa na vijana wa Chadema kwenye
makao makuu ya chama hicho wakati mwandishi huyo alipokwenda kupiga
picha maandamano ya vijana waliopinga kuondoka kwa katibu wa chama hicho
Dk Willbrod Slaa.
0 comments:
Chapisha Maoni