TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema wananchi wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga, hawatapiga kura ya kuchagua mbunge katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.
Hatua
hiyo, inatokana na kufariki dunia kwa aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo
hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mwamvuli
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mohamed Mtoi (39).
Mtoi,
alifariki dunia Jumamosi iliyopita baada ya gari lake alilokuwa
akisafiria kuacha njia na kupinduka kisha kudumbukia kwenye korongo
wilayani Lushoto.
Akizungumza
na mtandao huu jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva,
alisema sheria inaruhusu kama mgombea atafariki dunia wakati huu wa
uchaguzi uahirishwe.
“Wananchi
wa Lushoto hawatapiga kura ya mbunge Oktoba 25, tumeahirisha hadi hapo
baadaye tutakapowatangazia na chama husika kitapokuwa kimepata mgombea,” alisema Jaji Lubuva.
Kulingana
na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Zubery Mwombeji, Mtoi alipata
ajali katika eneo la Magamba Coast, Kata ya Magamba wilayani Lushoto.
Alisema
gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Miraj Nuru (43), likitokea Tarafa ya
Mlola kwenda Mkuzi baada ya kumaliza shughuli za kampeni.
0 comments:
Chapisha Maoni