test

Alhamisi, 3 Septemba 2015

Mgombea urais Chadema asema anajua vizuri mahitaji na kero za watanzania.


 
Mgombea urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa aendelea na kampeni za kunadi sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWA katika mkoa wa Rukwa na amewaomba watanzania kumpa dhamana ya kuleta mabadiliko ya kweli kwani uwezo huo anao na anachohitaji ni ushirikiano wao. 
 
Mh Lowassa akiambatana na viongozi na wanachama wa UKAWA baada ya kupata mapokezi makubwa ya aliyoanzia kwenye uwanja wa ndege wa Sumbawanga anazungumza na maelfu ya wananchi walijitokeza amesema anajua vizuri mahitaji na kero za watanzania na mahitaji nafasi ya kuziondoa.
 
Kuhusu tuhuma na hatua ya katibu wa Chadema Mh Wilbroad Slaa ya kujiengua mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe amesema chama kiko imara kwani ni sio mali ya mtu mmoja ni mali ya watanzania wote na hakuna muda wa kupoteza kwani watanzania wanahitaji na wako tayari kwa mabadiliko.
 
Mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga pamoja  na kuwaomba wananchi kumchagu Mh Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA ili waweze kuondoa kero za muda mrefu ikiwemo ya maji na huduma zingine za kijamii.
 

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni