Kwa ufupi
Taarifa zilizolifikia Mwananchi Digital zinasema majeruhi sita wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Tarime baada ya kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea jana kijijini Mangucha wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani kata ya Kegonga katika jimbo la Tarime Vijijini.
Dar es Salaam. Mtu mmoja amekufa, watano wamejeruhiwa katika vurugu zilizohusisha wafuasi wa CCM na Chadema katika jimbo la Tarime Vijijini.
Harakati za kisiasa katika jimbo la Tarime Mjini zimeshuhudia gari la mgombea ubunge wa Chadema, Esther Matiko likiharibiwa vibaya na watu waliokuwa wanapinga mabango yake kuwekwa eneo la CRDB mjini Tarime.
Muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Tarime, Rose Asea amekiri kupokea mwili wa mtu mmoja, wanne wengine wakilazwa kwa matibabu hospitalini hapo na kwamba mtu mmoja amepelekwa hospitali ya mkoa mjini Musoma kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kuwa mbaya.
Chanzo cha kuaminika kimesema, vurugu zilizuka katika kijiji cha Mangusha baada ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda kumlaki mgombea ubunge wa chama chao katika jimbo la Tarime Vijijini, John Heche aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni zao zilizokuwa zinafanyika katika kijiji cha Kegonga.
“Walipofika kijijini Mangucha walipita karibu na sehemu palipokuwa na mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani za CCM katika kata hiyo, ndipo vurugu zilipotokea” kilisema chanzo hicho.
Mjini Tarime, taarifa zinadai kuwa gari la mgombea Ubunge wa Chadema, Esther Matiko limeharibiwa vibaya na wananchi wanaoaminika kuwa wafuasi wa CCM baada ya kukutwa likiwa na mabango ya mgombea huyo barabara ya Nyamwaga karibu na benki ya CRDB.
Tukio hilo limetokea alfajiri leo wakati watu watatu waliokuwa kwenye gari hilo walipokuwa wanajiandaa kuweka mabango ya mgombea huyo wa Chadema kwenye eneo hilo la CRDB jambo ambalo liliwakera wafuasi hao wa CCM.
“Watu hao walilishambulia gari hilo kwa mapanga na kuharibu vioo na matairi” kilisema chanzo chetu cha kuaminika toka mjini humo, kiliongeza.
“Kama si polisi kuingilia kati tukio hilo lingeweza kusababisha maafa kwani wafuasi wa Chadema nao walianza kujibu mapigo kwa kung’oa mabango ya mgombea wake wa urais Dk John Magufuli” kilisema chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Vurugu hizo zimetokea eneo la jirani na viwanja vya Sabasaba ambavyo leo vitashuhudia mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk Magufuli ambaye taarifa za uhakika zinasema ameshawasili mjini humo toka Butiama alikohutubia mkutano wa kampeni jana.
Polisi wamethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kwamba watu wanne wanashikiliwa wakituhumiwa kuhusika na tukio la jana kijijini Mangusha. Upelelezi shauri la uharibifu wa gari la Matiko umeshaanza.
Jimbo jipya la Tarime mjini limekuwa katika mvutano mkubwa wa kisiasa ambapo mbunge wa kuteuliwa wa Chadema anayemaliza muda wake Esther Matiko anachuana vikali na Michael Kembaki wa CCM na Deo Meck wa ACT-Wazalendo.

0 comments:
Chapisha Maoni