Zaidi ya wananchi elfu nne wa Mkoa wa Arusha hasa Arumeru watagawiwa mashamba baada ya serikali kufuta umiliki wa wawekezaji wa baadhi ya mashamba waliyokuwa wanamiliki katika mkoa huo.
Hatua hiyo imetangazwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelezo ya Makazi William Lukuvi ambaye amesema zoezi la ufutaji milki ya mashamba yasiyotumika pia limefanyika Mkoa wa Morogoro ambako maeneo ya mashamba hayo yatagawiwa kwa wakulima na wafugaji.
Chanzo: ITV
0 comments:
Chapisha Maoni