HALI ya Umoja wa Vyama vinne vya Upinzani (UKAWA), si shwari ndani ya Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, kutokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na NCCR-Mageuzi kushindwa kuheshimu makubaliano ya kumsimamisha mgombea mmoja kwa kila kata.
Hali
hiyo imekuja baada ya wagombea udiwani wa Chadema kukataa kumuunga
mkono mgombea ubunge wa jimbo hilo NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ambaye
amesimama chini ya mwavuli wa Ukawa kwa madai kuwa, amekiuka makubaliano
ya umoja huo.
Wagombea
hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, katika kipindi hiki cha
kampeni, hawatamnadi mgombea ubunge wa Ukawa wakidai hata yeye mgombea
ubunge amekuwa akiwapiga vita wagombea udiwani wa Chadema.


0 comments:
Chapisha Maoni