test

Jumamosi, 12 Septemba 2015

BREAKING NEWS: Kubenea awashukia NEC..




Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Saed Kubenea amefichua mbinu za Tume ya uchaguzi (NEC) kukutana na mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Ukumbi wa Kilimanjaro Hoteli.

Kubenea amesema kuwa Maofisa wa tume hiyo walikutana na mgombea ubunge kupanga mbinu ya kutengeneza vitambulisho feki vya kupigia kura ameahidi kutaja jina lake wakati wa ufunguzi wa Kampeni za ubunge siku ya Jumapili.

Ameongeza kuwa wanajua njama zinazofanywa na NEC na watakuwa wanaweka wazi kila kitu ambacho tume hiyo katika mikutano yao ya kampeni alisema katika kampeni zao wataelezea madhaifu ya chama tawala kwa miaka 54.

Kubenea amesema kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM ameanza kufanya kampeni chafu ambapo aliandaa vijana feki wa chama hicho na kuwavalisha nguo za chadema na kuwaambia waandamane na kusema wanamuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilibroad Slaa.

Ameongeza kuwa tayari amemwagiza mwanasheria wake pamoja na wachama kupeleka malalamiko Nec ambayo wataambatanisha na Cd inayomuonyesha Mgombea huyo akiwa anajisifia kwa kitendo alichokifanya.

Amesema kitendo alichokifanya Masaburi ni kinyume na utaratibu wa maadili ya uchaguzi pia ameongeza kuwa kama wao wasivyochana mabango ya vyama vya upinzani nao wasichane ya kwao “Tutawachukulia hatua za kisheria vijana wanaopewa Sh 10,000 na wagombea kuchana mabango yetu kwa sababu tunaushaidi,”

Kubenea amemtupia lawama Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe kwa kuwatisha waangalizi wa Uchaguzi kutoa maoni, matokeo kabla ya NEC kutangaza matokeo na kusema mgombea wa CCM ndiye atakaye shinda.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni