test

Alhamisi, 27 Agosti 2015

Warioba: Magufuli ndiye kiongozi anayefaa



WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema Tanzania ya sasa inahitaji kiongozi mwadilifu, mzalendo na mchapakakazi kama alivyo mgombea wa CCM, Dk John Magufuli.
Jaji Warioba akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM jana Dar es Salaam, alisema Dk Magufuli ni mchapakazi kweli kweli na hana masihara anapokuwa ofisini au nje ya ofisi. “Wote mmemshuhudia akiwa Waziri wa Maendeleo ya Uvuvi, Ardhi na sasa hivi Ujenzi, amekuwa mchapakazi na amekuwa anawaelemisha wananchi wazifahamu haki zao,” alisema Jaji Warioba.
Dk Warioba alisema wakati alipokuwa mwenyekiti wa Tume ya Rushwa wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, alibaini kuwa sekta ya ujenzi ilikuwa inaongoza kwa rushwa, lakini tangu Dk Magufuli apewe wizara hiyo hakuna ufisadi tena.
Alisema kama Dk Magufuli angeamua kuchukua hata asilimia moja tu ya ujenzi wa Daraja la Mkapa, Daraja la Malagarasi au Daraja la Kigamboni angekuwa tajiri wa kutupa, lakini hakuwahi kujihusisha na vitendo hivyo vya kifisadi na ndio maana hana utajiri wowote.
“Tumesikia ufisadi wa EPA, Richmond, Escrow lakini hatujasikia ufisadi kwenye ujenzi na hii inadhihirisha kuwa Dk Magufuli ni mwadilifu,” alisema Jaji Warioba.
Jaji Warioba alisema mgombea huyo wa CCM ni mkali na hapendi kazi za ovyo ovyo, lakini pia anafuatilia kwa karibu.
Alisema chanzo cha ufisadi ni kutokana na viongozi kuwa karibu na matajiri, jambo ambalo mgombea huyo hana tabia hiyo.
Alisema mgombea huyo hana makundi badala yake kundi lake ni Watanzania wote hivyo akatoa mwito kwa Watanzania kumpa kura ili aweze kuwaongoza Watanzania na kuwaletea maendeleo ya kweli.
Aliongeza kuwa, atashiriki kumnadi mgombea huyo kwani anafahamu uadilifu wake “Leo ni siku ya uzinduzi, hatuwezi kusema mengi, lakini nitakuwa naye bega kwa bega na nitashiriki kuieleza ilani ya CCM kwa wapiga kura kwa nini wamchague Dk Magufuli.”

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni