Vijana wawili wenye uhusiano wa kimapenzi wamekamatwa na
kushitakiwa kwa kujaribu kujiunga na wanamgambo wa kundi la Islamic
State huko Syria. Muhammad Dakhalla mwenye umri wa miaka 22 na mpenzi
wake wa kike Jaelyn Young mwenye umri wa miaka 20 walikamatwa na maafisa
wa FBI jumamosi baada ya kusafiri hadi uwanja wa ndege wa Golden
Triangle ulioko Columbus, Mississippi wakiwa na kusudi la kupanda ndege
wakielekea Amsterdam na hatimae Istanbul.
Wawili hao wameshitakiwa kwa kupanga njama na kijaribu kutoa vifaa vya kusaidia Islamic State. Kwenye taarifa ya kiapo iliotolewa na afisa wa FBI, wote wawili wamekiri mashitaka baada ya kukamatwa. Kulingana na waraka wa malalamishi, vijana hao wawili walizungumza kwa njia ya mitandao na mawakala wa FBI, kwamba walikusudia kusafiri hadi Syria kusaidia kundi la Islamic State.

0 comments:
Chapisha Maoni