test

Ijumaa, 21 Agosti 2015

TFF: Yatangaza ratiba ya ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2015/2016.



Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza rasmi ratiba ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016, ambao utakuwa na jumla ya timu 16 badala ya 14 za msimu uliopita.
Ligi Kuu ya Bara imepangwa kuanza Septemba 12 mwaka huu, na itamalizika Mei saba mwakani, lakini itasimama kwa mapumziko kati ya Novemba saba na Desemba 19 mwaka huu, kupisha michuano mbalimbali ya kimataifa.

TFF imetangaza ratiba ya ligi hiyo, na kusema imezingatia ratiba ya mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, ambayo yatahusisha vilabu na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Lgi, Boniface Wambura, anaelezea kuhusu ratiba hiyo.

Wambura amezungumzia pia mashindano ya Kombe la FA, ambayo yamerejeshwa na TFF kwa jina la Kombe la Shirikisho.
Amesema mashindano hayo yatafanyika mwaka huu kwa kushirikisha timu za Ligi Daraja la Pili, la kwanza na Ligi Kuu, ili kumpata bingwa ambaye ataiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Wakati huohuo, TFF kupitia msemaji wake, Baraka Kizuguto, imezungumzia kukamilika kwa maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Yanga na Azam, ambao utachezwa Jumamosi mwishoni mwa wiki hii, na kuwataja waamuzu wa mchezo huo.

Mchezo wa Ngao ya Hisani baina ya Yanga na Azam, utachezwa kuzindua rasmi msimu mpya wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu wa mwaka 2015/2016.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni